Pata taarifa kuu
DRC RUFAA

DRC: Vital Kamerhe ahukumiwa kifungo cha miaka 13 gerezani katika kesi ya rufaa

Alihukumiwa mwaka jana kifung cha miaka 20 jela kwa kile kilichdaiwa kuwa wizi wa pesa za umma, Vital Kamerhe, mkuu wa zamani wa idaraya wafanyakazi waIkulu ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amethibitishwa kutiwa hatiani kwake. Wafuasi wa kingzi huy wamelaani vikali uamuzi huo amba wameuita wa kisiasa.

Vital Kamerhe mwanasiasa mashuhuri nchini DRC
Vital Kamerhe mwanasiasa mashuhuri nchini DRC AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Hukumu ilitlewa baada ya kusubiriwa kwa saa 7 jioni katika mahakama na ulikuwa mwisho wa mashaka kwa wakosoaji wa Vital Kamerhe - ambao walitarajia kurejeshwa kwa kifungo chake cha miaka ishirini gerezani - na pia kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakidai kuachiliwa kwake. Mahakama iliamua: miaka kumi na tatu gerezani.

Hukumu hiyo ilipingwa haraka na Jean-Marie Kabengele, wakili wa Vital Kamerhe. “Hatukubaliani na uamuzi huu, mteja wetu hastahili shida yoyote. Tutakuwa, baada ya kushauriana naye, tutajua ni njia gani itakayochukuliwa. "

Majaji walisimama kidete juu ya kutetea mamilioni ya dola zinazo daiwa kupitishwa mlang wa nyuma na kumba, marejesho ya zaidi ya dola milioni 50 zilizotapeliwa, na vile vile kukamatwa kwa mali na fedha zilizowekwa katika benki iwe kwa Kamerhe, mkewe na mabinti wawili wa mkewe.

 

Billy Kambale, katibu mkuu wa chama cha Vital Kamerhe, UNC.amesema  "Hukumu hii haiwezi kupingwa kwetu. Ni njama ya kisiasa ambayo haitapita kamwe. Hii inathibitisha kile tulichosema tangu mwanzo, ilikuwa njama za kisiasa. Na watu binafsi badala ya kusimamia Jamhuri hutumia wakati wao kusuluhisha akaunti na kiongozi mwakilishi zaidi wa Jamhuri. Uongozi wa kitaifa wa kisiasa wa chama changu utakutana na kutumia chaguzi hizo kwa sababu lazima wajue kuwa UNC itasimama katika njia yao. "

Upande wake Samih Jammal, mfanyabiashara wa raia wa Lebanoni, mmiliki wa kampuni za Samibo Congo na Husmal ambaye alikuwa amepata mikataba kwa makubaliano ya pamoja ya nyumba zilizopangwa tayari, adhabu yake ilipunguzwa kwa kiasi kikubwa kutoka miaka ishirini hadi miaka sita ya kazi ya kulazimishwa. Jeannot Muhima, msimamizi wa uagizaji na usafirishaji wa rais, pia aliona adhabu yake imepunguzwa kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja gerezani.

Wakati wa usiku, polisi walitawanya wanaharakati ambao walikuwa wamekusanyika karibu na makao makuu ya UNC Kinshasa kupinga uamuzi huo. UNC imebaki katika muungano na Rais Felix Tshisekedi licha ya kuhukumiwa kwa kiongozi wake kwa mwaka mmoja. Chama hicho kina wanachama watano katika serikali ya sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.