Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

DRC: Vital Kamerhe aachiliwa huru kwa muda

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mahakama imemwachilia huru kwa muda, Vital Kamerhe aliyekuwa Mkuu wafanyakazi katika Ikulu ya rais jijini Kinshasa kwa sababu za kiafya.Kamerhe aliyekuwa mshirika wa karibu wa rais Felix Thisekedi, alifungwa jela miaka 20  mwaka 2020, baada ya kubainika alifuja fedha za umma, karibu Dola Milioni 50. 

Vital Kamerhe, mkurugenzi wa zamani kwenye ofisi ya rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi.
Vital Kamerhe, mkurugenzi wa zamani kwenye ofisi ya rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Spika huyo wa zamani wa Bunge mwenye umri wa miaka 62, alipunguziwa kifungo mpaka miaka 13 jela baada ya kukataa rufaa, kuhusu kesi hiyo ya ufisadi iliyompata na kosa la ubadhirifu wa fedha za mpango wa kujenga maakazi ya maafisa wa usalama chini ya mpango wa serikali.

Wafuasi wa wachama chake cha UNC wamekuwa wakisherehekea kuachiwa kwa kiongozi wao, na baada ya tarifa hizo kutangazwa Jumatatu jioni, sherehe zilitanda katika makao makuu ya chama chake jijini Kinshasa.

Tunafuraha sana kumwona amepewa uhuru, yeyé ni kiongozi ambaye ametumikia sana nchi yake, tangu alipokuwa kijana.

Akizungumza na RFI Kiswahili, Alain Cuma, msemaji wa chama cha Kamerhe cha UNC jimboni Kivu kaskazini, alithibitisha kuwa kiongozi wao aliachiwa na yuko nyumbani kwake.  

Nakuhakikishia kuwa, Bwana Vital Kamerhe ametoja jela na yupo nyumbani kwake na kukutana na familia yake. 

Kabla ya kuachiwa huru, alipaswa kulipa Mahakamani Dola 500,000. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.