Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

DRC: Vital Kamerhe abadilishiwa hukumu ya kifungo cha miaka 13

Mahakama ya juu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imebadilisha hukumu ya Mahakama ya rufaa, iliyokuwa imemfunga miaka 13 jela Vital Kamerhe aliyekuwa mkuu wa utawala katika Ofisi ya Rais Felix Tshisekedi kwa kumpata na hatia ya matumizi mabaya ya fedha za umma. 

Vital Kamerhe, hapa alikuwa Gneva mnamo mwaka 2018.
Vital Kamerhe, hapa alikuwa Gneva mnamo mwaka 2018. © AFP - FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa Mahakama hiyo wamesema, baada ya kupokea rufaa ya Kamerhe kupinga hukumu aliyokuwa amepewa, imekubaliana na hoja zake na hivyo kufuta hukumu iliyokuwa imetolewa hapo awali. 

Aidha, Mahakama hiyo kwenye maamuzi yake imesema Jaji wa Mahakama ya rufaa, alivunja haki za upande wa utetezi kwa upande wa Kamerhe na wakati wa kesi hiyo, kulikuwa na pingamizi kuhusu Majaji waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo. 

Kesi hii sasa imerejeshwa kwenye Mahakama hiyo ya rufaa ya Gombe, kusikilizwa tena na Majaji wapya. 

Hii ndio Mahakama ambayo iliagiza kuwa mshirika huyo wa zamani wa rais Thisekedi aondolewe gerezani kwa muda ili apate matatibu kufuatia hali yake kuwa mbaya. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.