Changu Chako, Chako Changu
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Historia ya waswahili wa Burundi katika Makala Changu Chako Chako Changu na Ali Bilali
Katika Makala haya, Ali Bilali mtangazaji wa maswala ya Historia na utamaduni kutoka RFI Kiswahili anakuletea historia ya waswahili wa Burundi katika mazungumzo na mzee mkongwe mwana Historia kutoka Buyenzi, Mzee Anzuruni Hussein, ikiwa ni sehemu ya kwanza, na kwenye le Parler francophone tutaangazia kuhusu ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance Francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki tutamuangazia mwanamuziki Vichou Love kutoka nchini Burundi.27/08/202320:01 -
Wapemba wa Kenya wapewa vitambulisho vya uraia baada ya kutambuliwa
Ni furaha kubwa kwangu kukutana nawe kwa mara nyingine tena Jumapili ya leo katika Makala changu Chako Chako Changu, ambapo hivi karibuni rais wa Kenya aliwapa vitambulisho watu kutoka kabila la wapemba miezi kadhaa baada ya kuwaidhinisha kuwa miongoni mwa makabila ya wakenya, na kwenye le parler francophone nitakuletea ratiba ya shughuli kwenye Alliance francaise na Nairobi na Institut francais ya Lubumbashi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Ferre Golla Mimi ni Ali Bilali23/08/202319:51 -
Kina Mama kutoka kundi la Warumba wa Nyakanga nchini Burundi waeleza kuhusu utamaduni wao
Katika Makala haya Mtangazaji wako Ali Bilali wa idhaa ya Kiswahili ya RFI amezungumza na kina Mama kutoka kundi la Warumba wa Nyakanga, ambao hutoa burudani ya kuimba kwa kutumia ngoma maharufu "Msondo" huku wakitoa pia somo la mafunzo ya kumfunda mwali katika utamaduni wa waswahili wa Buyenzi. Na kwenye Muziki utampata Kijana Khalid msanii wa miondoko ya Taarab kutoka nchini Burundi mwenye lengo la kuinua muziki huo nchini Burundi.23/08/202319:57 -
Mila na tamaduni za watu wa Rumonge Kusini mwa Burundi, Andy Mwag msanii tishio jukwaani
Katika makala haya Jumapili ya leo Ali Bilali anakuletea mila na tamaduni za watu wa Rumonge kusini mwa Burundi, na kwenye muziki utamsikia msanii Andy Mwag mwanamuziki kutoka nchini Burundi ambae amekuwa tishio jukwaani katika muziki wa Live. Ambatana na mtangazaji wako mwanzo hadi tamati, na usiksahau kumfollow kwa instagram kwa kuandika23/08/202320:00 -
Vijana wa Uvira na harakati ya kukuza sanaa ya kuigiza filamu, mwanamuziki Force Gave
Makala haya ya leo Changu Chako Chako Changu mtangazaji wako wa maswala ya historia sanaa na utamaduni Ali Bilali ametembelea huko Uvira na kufanya mazungumzo kuhusu sanaa hii ya kuigiza katika eneo hilo, lakini pia utapata kumsikia mwanamuziki kutoka eneo hilo Mr Gave. Ambatana naye. usikosi pia kumfollow katika mitandao ya kijamii facebook na instagram @billy_bilali30/07/202319:57 -
Maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani na sherehe za miaka 13 ya rfi kiswahili sehemu ya tatu
Karibu kuwa nami jumapili hii katika Makala haya ya Changu chako Chako Changu ambapo Jumapili hii nakuletea sehemy atatu na ya mwisho ya makala kuhusu siku ya Kiswahili Duniani Julay 7 iliokwenda sanjari na maadhimisho ya miaka 13 ya rfi kiswahili ambapo Kundi la Less Wanyika liliburudisha. Mimi naitwa Ali Bilali Karibu ama bienvenue.23/07/202320:03 -
Sehemu ya pili ya makala kuhusu maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani
Karibu katika Makala haya Changu Chako Chako Changu ambapo jumapili ya leo tunaendeleza sehemu ya pili ya Makala kuhusu maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani, Ali Bilali ndio langu jina Karibu.22/07/202320:06 -
Maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani na miaka 13 ya rfi kiswahili sehemu 1 Julay 9 2023
Karibu katika Makala changu Chako Chako Changu ambayo leo ni maalum kabisa kuhusu siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili ambayo huadhimishwa kila ifikapo Julay 7 ambapo huu ni mwaka wa pili tangu kuanza kuadhimishwa kwa siku hii baada ya shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi Elimu na Utamaduni kuidhinisha siku hii ili kulinda tamaduni za waswahili siziji kupotea. Mimi naitwa Ali Bilali ambatana name mwanzo hadi Tamati.22/07/202320:00 -
Sehemu ya pili ya Makala kuhusu Tamasha la Marahaba Music Expo jijini Bujumbura
Naam mskilizaji wa RFI Kiswahili na mpenzi wa Makala changu chako karibu katika sehemu hii ya pili ya Makala kuhusu tamasha la Marahaba Music EXPO lililofanyika huko jijini Bujumbura nchini Burundi ambapo RFI Kiswahili iliwakilishwa nami Ali Bilali mtangazaji wa maswala ya Historia sanaa na Utamaduni. Kumbuka sehemu ya kwanza nilikueleza namna tamasha lilivyokuwa na kuzungumza na wadau mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Tamasha la Marahaba Music Expo sasa ambatana nami katika sehemu hii ya pili.01/07/202320:04 -
Tamasha la Marahaba Music Expo jijini Bujumbura msimu wa 5 lavunja rekodi
Wadau kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni wamekutana jjijini Bujumbura kuanzia Juni 20 hadi Juni 25 katika tamasha la Marahaba Music Expo lililojumuisha wasanii takriban 150 kutoka katika kila kona ya dunia kushiriki katika tamasha hilo la kimataifa lillilopata mafaanikio makubwa baada ya idadi kubwa ya watu kujitokeza ambapo awamu ya kwanza ilifanyika mjini kati ya pili Kanyosha na ya tatu ilifanyika Kinama. Muandishi wetu wa maswala ya sanaa na utamaduni Ali Bilali alikuwepo27/06/202319:58 -
Siku kuu ya Muziki ya kila Juni 21 na msanii Katoi wa Tabaka wa kundi la Mijikenda Jazz Band
Karibu katika Makala Changu chako changu Jumapili ya leo ambapo tunazungumzia hasa kuhusu siku kuu ya mUziki ya Juni 21, na msanii Katoi wa Tabaka na kwenye le parler francophone tutazungumzia kuhusu tole la nne la kuheshimlisha wanamuziki wa Bongo Fleva linaloandaliwa na Alliance francaise ya Dar es salaam, na kwenye Muziki nitakiuletea muziki wa Kataoi wa Tabaka and the Mujikenda Jazz Band mimi naitwa Ali Bilali Bienvenue et bon reveil matinale.18/06/202319:58 -
Muandishi wa vitabu Wanjiru M Thuku wa Kenya azindua kitabo chake, wadau wajitokeza kumuunga mkono
Karibu katika Makala changu chako chako changu, Jumapili ya leo tunazungumzia kuhusu uandishi wa vitabu, tutakuwa naye Bi Wanjiru Othuku aliezindua kitabu chake juma hili, na kwenye le parler Francophone tutazungumzia kuhusu ratiba za shughuli za kitamaduni Alliance Francaise ya Nairobi, na kwenye Muziki nitamzungumzia mwanamuziki Jux kutoka nchini Tanzania, mimi naitwa Ali Bilali Bienvenue, Karibu, na asubuhi njema, ama bon reveil matinale.10/06/202319:58 -
Historia ya Bendi ya Lelele Africa Music na shindano la filamu kwa kutumia simu ya mkononi
Jumapili hii katika Makala Changu changu chako chako changu, ambapo leo nakuletea historia fupi ya bendi ya Lelele AfricA Music pamoja na shindano la filamu kwa kutumia simu linalofanyika Huko Misri, na kwenye le parler francopjhone tutaangazia kuhusu tamasha la Mombasa Ocean Festival lilioandaliwa kwa ushirkinao na Unbalozi wa Ufaransa nchini Kenya na Somalia, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Afende Ready Kutoka hko Bukavu. kumbuka kutufollow pia kwa instagram @billy_bilali04/06/202320:00 -
Tamasha la kukuza utamaduni wa watu kutoka kabila la bashi huko Bukavu
Makala haya yanakuletea tamaduni za watu kutoka kabila la washi kupitia tamasha lililoandaliwa ili kuboresha na kukumbusha vizazi vya sasa kuhusu tamaduni zao, hii ikiwa ni awamu ya kwanza ambapo itaendelea kuhusisha pia makabila mengine lengo kuu hasa ni kudumisha mila na tamaduni. Kupitia Makala haya Ali Bilali amezeungumza na Wakili Placide kueleza zaidi kuhusu tamasha hilo. Usikosi pia kutufollow kwa Instagram @billy_bilali28/05/202320:00 -
Historia ya Arthur Firmin na tamasha la Lelele Africa Music Taarab kutoka Mombasa
Ni Jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya ya Changu Chako Chako Changu ambapo leo nakuletea historia ya Arthur Firmin mpiga picha wa zamani na mtaalamu wa kupanda milima Mkenya mwenye asili ya Uingereza, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance Francaise ya Nairobi, Dar es salaam. Na kwenye Muziki nitakuletea muziki wa bendi ya Lelele Africa Music Taarab kutoka Mombasa nchini Kenya Mimi naitwa Ali Bilali Bienvenue.21/05/202319:56
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.