Pata taarifa kuu
UCHAMBUZI-UCHUMI

Kiwanda cha mafuta Dangote: 'Hakutakuwa tena na matatizo ya usambazaji wa petroli Nigeria'

Rais Muhammadu Buhari amezinduwa rasmi siku ya Jumatatu Mei 22, 2023 kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta kilichojengwa na bilionea Aliko Dangote. 

Kiwanda kipya cha kusafisha mafuta cha bilionea Aliko Dangote kilichopo Ibeju-Lekki, Lagos, Nigeria, Mei 22, 2023.
Kiwanda kipya cha kusafisha mafuta cha bilionea Aliko Dangote kilichopo Ibeju-Lekki, Lagos, Nigeria, Mei 22, 2023. REUTERS - TEMILADE ADELAJA
Matangazo ya kibiashara

Huu ni uzinduzi wa kisiasa, wiki moja tu kabla ya Rais anayemmaliza muda wake Muhammadu Buhari kumkabidhi madaraka Rais mteule Ahmed Bola Tinubu. Mradi huu, wenye thamani ya karibu dola bilioni 20, utaenezwa kwa eneo lenye ukubwa wa zaidi ya heka 2,500 katika eneo la Lekki. Hasa, utafanya iwezekanavyo kusambaza mafuta kwenye vituo vya mafuta vya nchi. Benjamin Augé, mtafiti katika taasisi ya Ifri, mtaalamu wa masuala ya nishati na Nigeria, anafafanua masuala yanayohusu miundombinu hii.

RFI: Benjamin Augé, ni uwezo gani wa uzalishaji wa kiwanda hiki kilichojengwa na bilionea Aliko Dangote?

Benjamin Augé: Uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hiki cha kusafisha mafuta ambacho kitazalisha mapipa 650,000 kwa siku ni sawa na takribani mara mbili na nusu ya matumizi ya Nigeria. Nigeria hutumia takriban mapipa 200,000 ya mafuta kwa siku. Kwa hivyo, kwa kawaida kuanzia wakati kiwanda hiki cha kusafishia mafuta kitakapoweza kuchakata ghafi ya Nigeria, kusiwe tena na matatizo ya usambazaji nchini Nigeria. Hivi sasa, hali ni ngumu kwa sababu karibu bidhaa zote za petroli nchini Nigeria zinaagizwa kutoka nje.

RFI: Hata hivyo Nigeria tayari ina mitambo ya kusafishia mafuta. Je, miundombinu ya Aliko Dangote italeta mabadiliko gani?

Kuna viwanda vinne vya kusafishia mafuta nchini Nigeria, lakini vinafanya kazi vibaya, hasa katika eneo linalozalisha la Niger Delta. Viwanda hivi vinafanya kazi vibaya ingawa uwezo wao uliowekwa, ambao ni kusema uwezo wao wa kubadilisha petroli, ni mapipa 445,000 kwa siku, kwa hiyo mara mbili ya matumizi ya Nigeria. Kwa sababu, kumejengwa mitambo ya kusafisha mafuta ambayo haijaitunzwa. Kwa hiyo uwezo wake umeshuka.

RFI: Nigeria ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa mafuta barani Afrika. Walakini, uzalishaji wake unapungua na faida za kiuchumi hazifikii matarajio. Je, hii inaelezwaje?

Hii ni kutokana na sababu kadhaa. Moja ambayo ni ya utaratibu wa kisheria, yaani kwa zaidi ya miaka kumi, kuna sheria ya mafuta ambayo imekuwa ikijadiliwa katika ngazi ya Bunge na Seneti. Hatimaye ilipitishwa mwaka wa 2021. Na katika muongo huo wote, karibu hakukuwa na uwekezaji wowote, kulishuhudiwa hata makampuni makubwa ya jadi yakisitisha shughuli zao nchini Nigeria kama Total na Shell au Chevron na Exxon, ambazo ziliuza vibali vyao. Na pia kuna changamoto nyingine, ambayo ni suala la usalama katika eneo linalozalisha la Delta ya Niger: 2022 na 2023 ilikuwa miaka rekodi katika suala la wizi.

Mwishoni mwa 2022, ilikadiriwa kuwa karibu mapipa 450,000 kwa siku yaliibwa nchini Nigeria. Hii ni sawa na uzalishaji wa Gabon na Kongo kwa pamoja. Na kwa hivyo, bila shaka, mapato hupungua kwa sababu uzalishaji wa kisheria hupungua na hawawezi kufikia mgawo wao wa OPEC kwa sababu hiyo. Kwa hivyo sababu mbili: sababu ya kisheria ambayo ilisababisha kukosekana kwa uwekezaji na sababu ya usalama / wizi ambao ulisababisha kushuka kwa kiwango.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.