Pata taarifa kuu

Nigeria: Muhammadu Buhari azindua kituo kipya cha kuchimba mafuta

Nchini Nigeria, miezi michache kuelekea uchaguzi wa urais mwezi Februari mwaka ujao na wakati nchi ipo kwenye kipindi kigumu cha kiuchumi, rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari amezindua kituo kipya cha kuchimba mafuta kati ya majimbo ya Gombe na Bauchi, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. AP - Bayo Omoboriowo
Matangazo ya kibiashara

Buhari amesema, ana uhakika uchimbaji huo utasaidia kuimarisha uchumi wa nchi yake. 

Tunafurahishwa na ugunduzi wa mafuta, karibu mapipa Bilioni  moja na kiwango cha Bilioni 500 cha gesi katika eneo la Kolmani. Hii ni hatua kubwa…hii imesababisha kuvutia uwekezaji mkubwa kiuchumi kutokana na rasilimali hii…Miradi ambayo itafanyika ni pamoja na kusafisha mafuta, kujenga kituo cha  umeme na kile cha mbolea.Hii italeta mafanikio makubwa ya kitaifa na kuifanya nchi kuwa salama, kuwa na usalama wa chakula na kuiendeleza nchi kiuchumi. 

Hatua hii inakuja baada ya hivi karibuni Nigeria, kupoteza nafasi yake ya kwanza ya kuzalisha mafuta kwa sababu ya wizi wa mafuta, ufisadi na nafasi hiyo kuiendea Angola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.