Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Tume ya uchaguzi Nigeria yatiwa wasiwasi na mvutano wa kisiasa kuelekea uchaguzi

Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria (INEC) imesema leo Ijumaa "inatiwa wasiwasi"  kuhusu kuongezeka kwa ghasia wakati wa kampeni za uchaguzi, miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais na wa wabunge.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mahmood Yakubu anaonya kuwa, iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa, kuna uwezekano mkubwa wa machafuko hayo kuongezeka kuelekea uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mahmood Yakubu anaonya kuwa, iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa, kuna uwezekano mkubwa wa machafuko hayo kuongezeka kuelekea uchaguzi huo. © The Guardian Nigeria
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mahmood Yakubu ametoa taarifa hii baada ya kuripotiwa visa zaidi ya 50 kuhusiana na machafuko ya kisiasa, baada ya kuanza kampeni mwezi mmoja uliopita. 

Yakubu anaonya kuwa, iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa, kuna uwezekano mkubwa wa machafuko hayo kuongezeka kuelekea uchaguzi huo. 

Katika historia ya kampeni za kisiasa nchini humo, visa vya machafuko na vitisho huripotiwa wakati wa kampeni kama kipindi hiki. 

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa, hali hii itaendelea kushuhudiwa kwa sababu uchaguzi wa kumrithi rais Muhammadu Buhari unatarajiwa kuwa na ushindani mkali. 

Kinyang'anyiro kinatarajiwa kuwa kati ya Bola Tinubu wa chama tawala APC na Atiku Abubakar wa chama, cha PDP. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.