Pata taarifa kuu

Watoto ishirini waliotekwa nyara kaskazini-magharibi mwa Nigeria waachiliwa

Nchini Nigeria, wiki iliyopita, makumi ya watu wenye silaha wakiwa kwenye pikipiki walivamia shamba lililoko nje ya kijiji cha Mairuwa (Jimbo la Katsina) kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, na kuwateka nyara watoto 21 waliokuwa wakifanya kazi katika shamba hilo, kwa mujibu wa  msemaji wa polisi wa Katsina, Gambo Isah, na ofisa wa eneo hilo. Mateka wote wameachiliwa, polisi imetangaza leo Jumapili.

Wanawake waandamana kupinga ongezeko la visa vya utekaji nyara nchini Nigeria.
Wanawake waandamana kupinga ongezeko la visa vya utekaji nyara nchini Nigeria. REUTERS - AFOLABI SOTUNDE
Matangazo ya kibiashara

Polisi pamoja na wakaazi wa eneo hilo walikuwa wamesema watekaji nyara wanadai kulipwa fidia ili wawaachilie huru.

Katsina ni jimbo la Rais Muhammadu Buhari na ni miongoni mwa majimbo ya Kaskazini Magharibi na Kati ambako wahalifu waliojihami kwa silaha hutumia pikipiki kuwauwa wakaazi au kuwateka nyara na baadaye kudai fidia.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Gambo Isah amethibitisha tukio hilo lakini hakutoa taarifa zaidi.

Awali wakaazi walisema watoto hao walichukuliwa kutoka katika mashamba walikokuwa wakivuna mazao karibu na vijiji vya Mailafiya na Kurmin Doka katika jimbo hilo la Katsina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.