Pata taarifa kuu

Usalama waimarishwa nchini Nigeria baada ya tahadhari ya mashambulizi

Polisi ya Nigeria imetangaza kuimarisha ulinzi kote nchini, ambapo Marekani imewaamuru wanadiplomasia wasio wa lazima kuondoka Abuja, kutokana na "kuongezeka kwa hatari ya mashambulizi ya kigaidi" katika mji mkuu.

Washington imewaonya raia wake kwamba "magaidi wanaweza kushambulia" maduka makubwa, masoko, hoteli, migahawa, baa na shule katika mji mkuu. Nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Australia na Canada, zilitoa maonyo kama hayo lakini hadi Ijumaa asubuhi, zilikuwa bado hazijawahamisha wafanyakazi au familia zao kutoka Abuja.
Washington imewaonya raia wake kwamba "magaidi wanaweza kushambulia" maduka makubwa, masoko, hoteli, migahawa, baa na shule katika mji mkuu. Nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Australia na Canada, zilitoa maonyo kama hayo lakini hadi Ijumaa asubuhi, zilikuwa bado hazijawahamisha wafanyakazi au familia zao kutoka Abuja. AP - Chinedu Asadu
Matangazo ya kibiashara

Wakati chanzo cha tishio bado hakijajulikana, wakaazi wa Jimbo Kuu la Shirikisho (FCT) wamekuwa katika hali ya tahadhari tangu Jumapili baada ya balozi kadhaa za Magharibi kutoa maonyo ya kuwashauri raia wao kupunguza kusafiri kwenda Nigeria, nchi yenye watu wengi zaidi Afrika.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi jioni, polisi ya Nigeria ilitoa wito kwa maafisa wake wakuu wote "kuimarisha usalama katika maeneo yao, hasa katika FCT." Inspekta Jenerali wa Polisi Usman Alkali Baba aliwataka wakazi wa eneo hilo lenye wakazi milioni sita "kuwa waangalifu na kuripoti polisi matukio yoyote yenye mashaka au yasiyo ya kawaida".

Siku ya Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza kuwa imewaamuru wafanyakazi wake wasio wa lazima walioko Abuja kuondoka katika jiji hilo. Ubalozi wa Marekani nchini Nigeria, kwa upande wake, unaonyesha kwamba agizo hilo linahusu familia za maafisa wote wa Marekani nchini humo.

Washington imewaonya raia wake kwamba "magaidi wanaweza kushambulia" maduka makubwa, masoko, hoteli, migahawa, baa na shule katika mji mkuu. Nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Australia na Canada, zilitoa maonyo kama hayo lakini hadi Ijumaa asubuhi, zilikuwa bado hazijawahamisha wafanyakazi au familia zao kutoka Abuja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.