Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Boti yazama nchini Nigeria baada ya mafuriko, watu wengi watoweka

Watu "wengi" wametoweka na 15 wameokolewa baada ya boti kuzama kusini mashariki mwa Nigeria, eneo lililokumbwa na mafuriko makubwa, huduma za dharura zilisema siku ya Jumamosi.

Wani mai sayar da takalma yayin tura kararsa a kan daya daga cikin titunan Maiduguri da ambaliyar ruwa ta mamaye a Najeriya, 5 ga Yuli, 2017.
Wani mai sayar da takalma yayin tura kararsa a kan daya daga cikin titunan Maiduguri da ambaliyar ruwa ta mamaye a Najeriya, 5 ga Yuli, 2017. © STEFAN HEUNIS/AFP/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Boti hiyo ilizama siku ya Ijumaa huko Umunnankwo katika Manispaa ya Ogbaru, iliyoko kwenye Mto Niger katika Jimbo la Anambra. "Haijabainika ni watu wangapi walikuemo katika boti hiyo," Chukwudi Onyejekwe, afisa wa huduma za dharura za serikali, ameliambia shirika la habari la AFP.

“Tumeokoa watu 15 na wengine wengi hawajulikani walipo,” ameongeza.

Amesema hadi sasa hakuna maiti iliyopatikana na kwamba shughuli za utafutaji zinaendelea.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, watu 85 walikuwa wamepanda boti hiyo.

Maeneo mengi ya Nigeria yameathiriwa tangu kuanza kwa msimu wa mvua kutokana na mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya watu 300 na wengine 100,000 kukosa makazi, kulingana na huduma za dharura. Maeneo makubwa yanayolimwa yameharibiwa na hivyo kuzua hofu ya kuongezeka kwa uhaba wa chakula nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.