Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Nigeria: Wagombea urais wajiandaa kwa miezi 5 ya kampeni

Serikali ya Nigeria itatangaza kuanza kwa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais siku ya Jumatano. Wagombea 18 walio kwenye mstari wa kuanzia wana matumaini baada ya miezi mitano ya kampeni ya kuchukua uongozi wa nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika wakati ambapo inapitia mzozo mkubwa wa kiuchumi na kiusalama.

Mojawapo ya mada kuu ya uchaguzi wa rais wa 2023 ni hali maalum ya Nigeria: "kugawa maeneo". Kulingana na makubaliano haya ya kimya kimya, uchaguzi wa urais lazima ubadilishe kila mihula miwili kati ya mgombea kutoka kaskazini, hasa Mwislamu, na kutoka kusini, hasa Mkristo.
Mojawapo ya mada kuu ya uchaguzi wa rais wa 2023 ni hali maalum ya Nigeria: "kugawa maeneo". Kulingana na makubaliano haya ya kimya kimya, uchaguzi wa urais lazima ubadilishe kila mihula miwili kati ya mgombea kutoka kaskazini, hasa Mwislamu, na kutoka kusini, hasa Mkristo. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kuchukua nafasi ya Rais Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 79, ambaye hatagombea tena uchaguzi mwishoni mwa mihula yake miwili, wagombea wawili wakuu wanashindana. Hao ni Atiku Abubakar, wa chama cha People's Democratic Party (PDP), na Bola Ahmed Tinubu, wa chama tawala, Congress of Progressives (APC).

Lakini miezi mitano kabla ya uchaguzi, hakuna mtu anayepewa nafasi ya kushinda uchaguzi huo, na ni nadra kwa taifa hilo kubwa la Afrika Magharibi ambalo liliingia katika mfumo wa demokrasia mwaka 1999, wagombea wa vyama viwili vikuu hawaonekani kuwa na uhakika wa kuweza kushinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

“Tofauti na chaguzi sita zilizopita, uchaguzi wa mwaka 2023 hazitakuwa za wagombea wawili,” amesema Profesa Dapo Thomas wa Chuo Kikuu cha Lagos.

Tajiri na mwenye utata

Bw. Tinubu na Bw. Abubakar, ambao wote wana umri zaidi ya miaka 70, na matajiri wa kupindukia na wenye utata, watalazimika kuwashawishi wapiga kura katika nchi ambayo asilimia 60 ya watu ni chini ya miaka 25, na ambapo inazidi kuongezeka chuki dhidi ya tabaka la wazee, tabaka la kisiasa linalotuhumiwa kwa ufisadi na utawala mbovu.

Pia, mgombea ambaye si maarufu ameibuka katika miezi ya hivi karibuni. Huyu ni Peter Obi wa chama cha Labour, gavana wa zamani ambaye anapendwa sana na vijana na ambaye anafurahia uungwaji mkono mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

"Lakini mafanikio haya kwa vyombo vya habari hayamaanishi kuwa uchaguzi utakuwa wa urahisi," linabainisha shirika la Eurasia, linalohusika na kutafakari. Linahoji kuhusu uwezo wa Bw. Obi na chama chake "kuweza kuanzisha, chini ya miezi sita", mtandao wenye uwezo wa kuhamasisha "wapiga kura katika karibu vituo 180,000 vya kupigia kura nchini kote".

Nchini Nigeria, waliojitokeza kupiga kura kwa ujumla ni wachache (33% katika uchaguzi wa urais wa 2019) na vijana sio wapiga kura wanaoshiriki zaidi.

Siasa pia inategemea kwa kiasi kikubwa kuungwa mkono na mamilioni ya dola ambazo wagombea wanaweza kuwekeza katika kampeni.

Jumla ya wagombea 18 akiwemo mwanamke mmoja wanashiriki. Upigaji kura utafanyika Februari 25. Wananchi wa Nigeria pia watachagua wawakilishi wao bungeni tarehe hii.

Kampeni hiyo ambayo itafunguliwa rasmi siku ya Jumatano itachukua muda wa miezi mitano, ambayo wachambuzi wanasema inaweza kuzidisha mizozo ndani ya vyama na kuzidisha migawanyiko katika nchi ambayo tayari ina mgawanyiko mkubwa kati ya Waislamu wa kaskazini na Wakristo wa kusini.

Mgawanyiko kati ya kaskazini na kusini

Mojawapo ya mada kuu ya uchaguzi wa rais wa 2023 ni hali maalum ya Nigeria: "kugawa maeneo". Kulingana na makubaliano haya ya kimya kimya, uchaguzi wa urais lazima ubadilishe kila mihula miwili kati ya mgombea kutoka kaskazini, hasa Mwislamu, na kutoka kusini, hasa Mkristo.

Kanuni hii inalenga kudumisha uwiano katika nchi yenye makabila zaidi ya 250 na ambapo mivutano kati ya jamii ni ya mara kwa mara.

Kwa sababu Rais Buhari anatoka kaskazini, nafasi ya urais inapaswa kuendeshwa na mgombea kutoka kusini. Lakini PDP ilichagua kupuuza "kugawa maeneo" kwa kumteua Bw. Abubakar, kutoka kaskazini mashariki.

Aidha, chama tawala, APC, kinatoa tikiti ya "Muslim Muslim". Bw. Tinubu, Mwislamu kutoka kusini, alichagua mgombea mwenza kutoka dini yake.

Jukumu linaonekana kuwa gumu kwa gavana huyu wa zamani wa Lagos ambaye kwa hakika ana ushawishi mkubwa, lakini ambaye lazima awe na ripoti mbaya ya miaka minane ya uongozi wa Bw. Buhari.

Nigeria imekuwa ikipitia mzozo mkubwa wa kiuchumi tangu janga la corona, kisha mashalbulizi ya Urusi nchini Ukraine, ambayo yamesababisha bei ya chakula na mafuta kupanda juu.

Uzalishaji wa mafuta unaendelea kudorora katika nchi hiyo ambayo imepoteza nafasi yake ya kuongoza kwa uzalishaji wa dhahabu nyeusi katika bara la Afrika katika miezi ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.