Pata taarifa kuu

Watawa wanne waliotekwa nyara nchini Nigeria waachiliwa

Watu wenye silaha wamewaachilia watawa wanne waliowateka nyara kusini mashariki mwa Nigeria siku ya Jumapili, polisi imesema leo Jumatano.

Katika miezi ya hivi karibuni, viongozi wa dini wamekuwa wakilengwa zaidi na wahalifu, sio kwa sababu za kidini au kiitikadi, lakini kwa sababu Kanisa linaonekana kuwa na uwezo wa kuhamasisha waamini kulipa fidia.
Katika miezi ya hivi karibuni, viongozi wa dini wamekuwa wakilengwa zaidi na wahalifu, sio kwa sababu za kidini au kiitikadi, lakini kwa sababu Kanisa linaonekana kuwa na uwezo wa kuhamasisha waamini kulipa fidia. AP - Rahaman A Yusuf
Matangazo ya kibiashara

Watawa hao wanne, waliotekwa nyara karibu na mji wa Okigwe katika jimbo la Imo, waliachiliwa Jumanne, msemaji wa polisi katika jimbo la Imo Michael Abattam amesema. Ameongeza kuwa watawa hao "wako salama salimini" lakini hakusema ikiwa fidia ililipwa ili kuweza kuachiliwa kwao.

Visa vya utekaji nyara hutokea mara kwa mara katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, iliyokumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na kukabiliwa na uhalifu unaokaribia kuwa wa jumla. Ingawa mateka wengine wakati mwingine huuawa, wengi huachiliwa baada ya malipo ya fidia.

Katika miezi ya hivi karibuni, viongozi wa dini wamekuwa wakilengwa zaidi na wahalifu, sio kwa sababu za kidini au kiitikadi, lakini kwa sababu Kanisa linaonekana kuwa na uwezo wa kuhamasisha waamini kulipa fidia.

Eneo la Kusini-mashariki mwa Nigeria pia linakabiliwa na ongezeko la ghasia zinazofanywa na kundi la watu wanaotaka kujitengwa kwa eneo la Biafra (Ipob). Kundi la Ipob, ambalo linataka kufufua jimbo tofauti la kabila la Igbo, limekanusha mara kwa mara kuhusika na ghasia katika eneo hilo.

Kutangazwa kwa uhuru na Jamhuri ya Biafra kulisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 30 kati ya mwaka 1967 na 1970. Vita hivyo vilisababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja, wengi wao kutoka jamii ya Igbo, na wengi walifariki kutokana na njaa na magonjwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.