Pata taarifa kuu

Watawa wanne watekwa nyara na watu wenye silaha nchini Nigeria

Watu wenye silaha waliwateka nyara watawa wanne wa Kikatoliki siku ya Jumapili katika Jimbo la Imo, kusini-mashariki mwa Nigeria ambako utekaji nyara kwa ajili ya fidia ni jambo la kawaida, polisi wamesema Jumatatu.

Vikosi vya usalama vya Nigeria vinawashikilia wanaume watatu waliotambuliwa kama watekaji nyara wa wanafunzi mnamo Septemba 23, 2021 huko Abuja.
Vikosi vya usalama vya Nigeria vinawashikilia wanaume watatu waliotambuliwa kama watekaji nyara wa wanafunzi mnamo Septemba 23, 2021 huko Abuja. AP - Gbemiga Olamikan
Matangazo ya kibiashara

 

"Watawa wanne kutoka Kanisa Katoliki wametekwa nyara," msemaji wa polisi wa Imo Michael Abattam ameliambia shirika la habari la AFP. Bw Abattam amedai kuwa watawa hao walitekwa nyara siku ya Jumapili karibu na mji wa Okigwe wakielekea kwenye misa. "Tuko tunawatafuta watekaji nyara kwa lengo la kuwaachilia waathiriwa," ameongeza.

Bado hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na utekaji nyara huo. Visa vya utekaji nyara hutokea mara kwa mara katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, iliyokumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na kukabiliwa na uhalifu unaokaribia kuwa wa jumla. Ingawa mateka wengine wakati mwingine huuawa, wengi huachiliwa baada ya malipo ya fidia.

Eneo la Kusini-mashariki mwa Nigeria pia linakabiliwa na ongezeko la ghasia zinazotekelezwa na Vuguvugu linadai kulotetea Uhuru kwa wakazi wa Biafra (Ipob). Ipob, ambayo inataka kuona kunaanzishwa  jimbo lililogawanyika kwa kabila la Igbo, imekanusha mara kwa mara kuhusika na ghasia katika eneo hilo.

Kutangazwa kwa uhuru na Jamhuri ya Biafra kulisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 30 kati ya 1967 na 1970. Vita hivyo vilisababisha vifo vya zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa kutoka jamii ya Igbo, huku wengi wao wakikabiliwa na njaa na magonjwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.