Pata taarifa kuu

Nigeria: Mfumuko wa bei wapanda hadi kiwango cha juu zaidi katika miaka 17

Uchumi wa Nigeria unazidi kudorora, huku mfumuko wa bei kwa ujumla ukifikia 19.6% mwezi Julai, kulingana na Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu. Jumanne hii, Agosti 17, thamani ya sarafu ya taifa, Naira, pia ilishuka dhidi ya dola.

Katika moja ya mitaa huko Lagos, Nigeria.
Katika moja ya mitaa huko Lagos, Nigeria. AFP - PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Raia wa Nigeria wamejikuta matatani baada ya kupanda kwa bei na sarafu inayozidi kushuka thamani. Gharama zinaongezeka katika sekta zote: nishati, usafiri, lakini pia chakula, kutokana na mlipuko wa bei ya mkate na nafaka.

Hata ukiondoa bidhaa muhimu zaidi, mfumuko wa bei unaendelea kupanda. Usimamizi mbaya wa kimuundo na wizi kwenye mabomba ya mafuta umezuia Nigeria kunufaika kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika miezi ya hivi karibuni.

Kinyume chake, ruzuku kubwa kwa bei ya petroli ni mzigo kwa bajeti ya serikali. Kwa mafuta yake, kama ilivyo kwa bidhaa nyingine nyingi za matumizi, Nigeria inategemea kabisa uagizaji wa bidhaa kutoka nje na kwa hiyo dola ya Marekani.

Waagizaji wanapata shida kubwa katika kupata fedha za kigeni, kutokana na vikwazo vya Benki Kuu, ambayo inalinda kwa umakini akiba yake ya ukwasi. Siku ya Jumanne, Sarau ya Nigeria iliporomoka, ambapo naira 683 iliuzwa dola 1 kwenye soko lisilo kuwa rasmi, chini ya 20% ya thamani yake kwenye kwenye benki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.