Pata taarifa kuu

Uongozi wa juu wa kijeshi wafanya mageuzi katika jeshi la Nigeria

Nchini Nigeria, mkuu wa majeshi ametoka tu kufanya mabadiliko makubwa ya maafisa wakuu. Miezi saba kabla ya uchaguzi wa rais, ukosefu wa usalama bado ni changamoto kubwa kwa Rais Muhammadu Buhari, ambaye aliahidi kukomesha uasi wa kijihadi.

 Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. © Nigeria presidency
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa uongozi wa juu wa kijeshi wanasema, mageuzi mapya na uteuzi ndani ya jeshi unalenga kuliweka sawa jeshi ili kufikia ufanisi wa shughuli zake.

Mabadiliko haya yanaathiri baadhi ya maafisa wa makao makuu ya jeshi, maafisa wakuu, makamanda wa jeshi, makamanda wa taasisi za mafunzo, makamanda wa brigedi, miongoni mwa wengine.

Sadeeq Garba Shehu, afisa wa zamani wa jeshi ambaye sasa amestaafu, anaeleza kuwa "ni mabadiliko ya kiutawala. Hayana uhusiano wowote na operesheni za jeshi. Lakini ukiangalia kwa makini orodha hiyo, tunaona mabadiliko katika uongozi wa jeshi yakimlenga jenerali aliyekuwa akisimamia shughuli katika Jimbo la Kaduna. Jimbo la Kaduna ni miongoni mwa majimbo ambayo yana matatizo ya kiusalama. Hivyo kwangu mimi haya ndiyo mabadiliko pekee, amesema.

Shambulio la hivi majuzi katika gereza la Kujé, karibu na mji mkuu Abuja, lilifuatia saa chache tu za shambulio la kuvizia kwenye msafara wa magari ya usalama wa Rais Muhammadu Buhari katika jimbo lake la Katsina.

Matukio haya mawili yanaongeza uhasama wa umwagaji damu kati ya Boko Haram na kundi la Islamic State huko Afrika Magharibi, visa vingi vya utekaji nyara kwa ajili ya fidia, bila kusahau harakati za kujitenga katika Delta ya Niger na eneo la Kusini-mashariki. Hali hii inayotokea inaonyesha ukubwa wa tishio la usalama nchini.

Yahuza Ketso, mtaalam wa masuala ya usalama, pia anatilia shaka ukweli wa mabadiliko haya ndani ya jeshi kutokana na hali halisi ilivyo sasa. "Sioni chochote kikubwa katika mageuzi haya mapya," anasema. "Lakini tuna mashaka kuona nini kitatokea."

Kwa hivyo usalama unasalia kuwa suala kuu katika uchaguzi mkuu na ule wa urais wa mwaka 2023 wa kumchagua mrithi wa Rais Buhari ambaye, baada ya mihula miwili ya uongozi wa nchi, hawezi tena kuwa mgombea.

Mabinti wa Chibok bado hawajapatikana isipokuwa tu baadhi yao walipatikana kwa idadi ndogo. Hivi majuzi treni ya abiria ilishambuliwa karibu na kituo cha Rijana, kinachounganisha Abuja na Kaduna, mji ulioko kaskazini-magharibi, karibu abiria 100 walitekwa nyara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.