Pata taarifa kuu
UCHUMI-SIASA

Uhaba wa noti za pesa nchini Nigeria: Maandamano mapya yaibuka Ibadan

Umati watu wenye hasira wamechoma matairi na kufunga barabara katika mji wa Ibadan, mji mkuu kusini magharibi mwa Nigeria, siku ya Jumatano kupinga uhaba wa noti za pesa ambao unadhoofisha nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, kulingana na polisi na wakaazi.

Katika wiki tatu zilizopita, ghasia zimezuka huko Ibadan, Abeokuta (kusini-magharibi) na Kano, jiji kubwa zaidi la kaskazini, baada ya uamuzi madhubuti wa Benki Kuu wa kuondoa noti za zamani za naira na kuweka noti mpya.
Katika wiki tatu zilizopita, ghasia zimezuka huko Ibadan, Abeokuta (kusini-magharibi) na Kano, jiji kubwa zaidi la kaskazini, baada ya uamuzi madhubuti wa Benki Kuu wa kuondoa noti za zamani za naira na kuweka noti mpya. REUTERS - Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa zikiwa zimesalia siku 10 kabla ya uchaguzi wa urais, foleni zinaendelea kuongezeka kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) kote nchini, jambo linalozidi kuwaelemea Wanigeria ambao tayari wamekumbwa na uhaba wa mafuta mara kwa mara.

Katika wiki tatu zilizopita, ghasia zimezuka huko Ibadan, Abeokuta (kusini-magharibi) na Kano, jiji kubwa zaidi la kaskazini, baada ya uamuzi madhubuti wa Benki Kuu wa kuondoa noti za zamani za naira na kuweka noti mpya.

Siku ya Jumatano, polisi wa jimbo la Oyo imesema maandamano yalizuka katika sehemu za Ibadan, mji mkuu wa jimbo hilo, asubuhi lakini yakadhibitiwa haraka. "Kulikuwa na maandamano asubuhi ya leo na baadhi ya wateja wa benki walikuwa na kinyongo," msemaji wa polisi Adewale Osifeso ameliambia shirika la habari la AFP.

Kulingana na wakaazi, machafuko hayo yalianza katika vitongoji kadhaa wakati wateja hao wenye hasira walipopinga kwamba hawawezi kutoa pesa zao benki au hawaweza kubadilisha noti zao za zamani kwa noti mpya.

"Barabara kuu zilifungwa, huku benki, maduka na biashara zingine zikifungwa," mwandishi wa habari wa eneo hilo Remi Feyisipo ameliambia shirika la habari la AFP, akiongeza, waandamanaji hao pia walikuwa na hasira kwa sababu wenye maduka na vituo vya petroli hawakubali tena noti za zamani.

Mnamo Oktoba, Benki Kuu ilitangaza ghafla kuwa inabadilisha noti (pamoja na rangi yao), na kuamua kuwa noti za zamani hazitakuwa halali tena mwishoni mwa mwezi Januari. Kisha ilisogeza mbele tarehe hiyo hadi Februari 10, kutokana na uhaba na shinikizo la raia.

Ni katika muktadha huo wa hasira za kijamii ambapo zaidi ya wapiga kura milioni 93 wametakiwa kupiga kura ili kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye anamaliza muhula wake wa pili kwa rekodi iliyokithiri kwa ukosefu wa usalama, ambao umekaribia kuwa wa jumla, na mgogoro wa kiuchumi.

Chama tawala kilihalalisha mabadiliko haya ya sarafu kwa hitaji la kupigana dhidi ya ununuzi wa kura, lakini upinzani unakituhumu kwa kuchukua uamuzi huu ili kuunyima uwezo na kuuzuia kufanya kampeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.