Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mlipuko wa 'bomu' waua watu ishirini na saba nchini Nigeria

Wafugaji 27 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa siku ya Jumatano katika mlipuko wa "bomu" katikati mwa Nigeria, eneo linalokumbwa na ghasia za kijamii, kwa mujibu wa polisi, wakati shirika la wafugaji likishtumu jeshi la anga kufanya shambulio la angani dhidi ya watu kutoka jamii yao.

Migogoro kati ya wafugaji na wakulima kuhusu ardhi, malisho na haki ya maji ni ya kawaida katika mikoa ya kati na kaskazini magharibi mwa Nigeria. Wiki iliyopita, watu tisa waliuawa na watu wenye silaha karibu na kambi ya watu waliokimbia makazi yao, kulingana na mamlaka ya jimbo la Benue.
Migogoro kati ya wafugaji na wakulima kuhusu ardhi, malisho na haki ya maji ni ya kawaida katika mikoa ya kati na kaskazini magharibi mwa Nigeria. Wiki iliyopita, watu tisa waliuawa na watu wenye silaha karibu na kambi ya watu waliokimbia makazi yao, kulingana na mamlaka ya jimbo la Benue. © Goran Tomasevic Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wafugaji na mifugo yao walikuwa katika kijiji cha Rukubi, mpakani mwa majimbo ya Nasarawa na Benue wakati "bomu" lilipolipuka katikati yao.

"Tumebaini kuwa watu 27 wameuawa katika mlipuko huo wa bomu pamoja na idadi kubwa ya mifugo," amesema afisa wa polisi wa jimbo la Nasarawa Maiyaki Muhammed Baba. "Watu wengine kadhaa walijeruhiwa na idadi ya vifo inaweza kuongezeka," ameongeza.

Wataalamu wa polisi wanachunguza chanzo cha mlipuko huo. Kwa upande wake, kundi linalowakilisha wafugaji limedai kuwa mlipuko huo ulitokana na shambulizi la jeshi la Nigeria.

'Shambulio la angani'?

"Lilikuwa shambulio la angani. Liliwaua watu 27" kutoka kundi la wafugaji, amesema Lawal Dano wa shirika la wafugaji wa Ng'ombe nchini Nigeria, Miyetti Allah. "Sote tunajua kuwa ni wanajeshi pekee ndio wana ndege za kufanya mashambulizi ya angani, na tunatoa wito wa uchunguzi wa kina na vikwazo muhimu kwa wale wanaohusika na tukio hili," afisa huyo ameongeza.

Katika siku za nyuma, kumekuwa na mashambulizi ya kijeshi kwa yanayo lenga bahati mbaya raia kaskazini mwa nchi ambapo jeshi linapambana na wanajihadi na magenge ya uhalifu.

Mnamo Septemba 2021, shambulio la angani la jeshi lilipiga kimakosa kijiji katika Jimbo la Yobe, na kuua takriban raia tisa. Jeshi la Wanahewa lilieleza kuwa ndege zake wakati huo zilikuwa zikifuata kundi la wanajihadi.

Na mwezi wa Januari 2017, takriban watu 112 waliuawa wakati ndege ya kijeshi ilipotekeleza shambulizi la angani dhdi ya kambi ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia za wanajihadi katika mji wa Rann karibu na mpaka na Cameroon. Katika ripoti iliyochapishwa miezi sita baadaye, jeshi lilielezea kosa hili kwa "kukosekana kwa alama sahihi za eneo hilo".

Migogoro kati ya wafugaji na wakulima kuhusu ardhi, malisho na haki ya maji ni ya kawaida katika mikoa ya kati na kaskazini magharibi mwa Nigeria. Wiki iliyopita, watu tisa waliuawa na watu wenye silaha karibu na kambi ya watu waliokimbia makazi yao, kulingana na mamlaka ya jimbo la Benue.

Mivutano hiyo, ambayo chimbuko lake ni zaidi ya karne moja, inasababishwa na ukame, ongezeko la watu, kupanuka kwa kilimo cha kukaa kimya na utawala mbovu. Katika miaka ya hivi karibuni, migogoro hii wakati fulani imechukua mwelekeo wa kikabila na kidini, huku wafugaji wa Fulani wakiwa Waislamu na wakulima wengi wao wakiwa Wakristo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.