Pata taarifa kuu

Nigeria: Mahakama Kuu yaongeza muda wa uhalali wa noti za zamani za Naira

Mahakama Kuu imeongeza Ijumaa muda wa uhalali wa noti za zamani pesa za Naira nchini Nigeria, na kubatilisha maagizo ya serikali ambayo imesababisha uhaba mkubwa wa pesa kwa wiki katika nchi yenye watu wengi barani Afrika.

Noti za pesa za Nigeria, Naira, zinaonekana kwenye picha hii, Septemba 10, 2018.
Noti za pesa za Nigeria, Naira, zinaonekana kwenye picha hii, Septemba 10, 2018. REUTERS - Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Katika uamuzi uliotolewa Ijumaa, Mahakama Kuu inadai kwamba Rais Muhammadu Buhari, ambaye serikali yake iliamua kufuta noti za Naira za zamani kuanzia mwezi Februari , alifanya bila mashauriano, hali ambayo "inamfanya kuwa dikteta".

Mnamo mwezi Oktoba, mamlaka nchini Nigeria ilitangaza ghafla mageuzi ya baadaye ya noti (kwa rangi), na iliamua kwamba noti hizo za zamani hazitakuwa halali tena mwishoni mwa mwezi wa Januari, tarehe ambayo ilisogezwa mbele hadi Februari 10 kwa sababu ya uhaba na na maandamano ya raia.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja, foleni kubwa zimetanda mbele ya benki, ambazo haziwezi kutoa noti mpya kwa idadi ya kutosha, na kusababisha raia, ambao nusu yao huishi katika umaskini uliokithiri, katika shida kubwa. Wanigeria wengi hufanya kazi katika sekta isiyo rasmi ya uchumi na hutumia pesa tu kwa shughuli zao za kila siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.