Pata taarifa kuu

Nigeria: Uhaba wa noti mpya kero kwa raia kuelekea uchaguzi mkuu

NAIROBI – Siku moja kabla ya raia wa Nigeria hawajapiga kura kuchagua rais na wabunge, uhaba wa noti mpya umeendelea kuwatatiza wananchi, hata kwa wale ambao hufanya miamala ya simu hali inayoathiri uchumi wa taifa hilo, raia wengi wakionekana kuchoshwa.

Uhaba wa noti mpya nchini Nigeria kuelekea uchaguzi mkuu wa Jumamosi
Uhaba wa noti mpya nchini Nigeria kuelekea uchaguzi mkuu wa Jumamosi © REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Nyuso za raia kweney foleni kwenye benki mbalimbali na waliojaa wasiwasi zitoa ishara tosha kwamba raia nchini Nigeria wamechshwa na uhaba wa kutafuta sarafu mpya, Gloria Mamadu anasema amepanga foleni kwa saa nane kutafuta dolla 10.

“Jana singeweza hata kutoa dolla mbili pekee, nilipanga foleni kutoka Saa kumi na moja alifajiri hadi 6 jioni, hapakuwa na pesa, hakuna, nataka haya yote yakome, hali hii inazidi.”amesema Glory Mamadu. 

00:11

Gloria Mamadu, Raia wa Nigeria

Raia Rome Williams, anayestaafu yeye ana maono tofauti kuhusiana na kinachoendelea kwa sasa, anaunga mkono matumizi ya pesa kutumia simu.

“kwa sasa mtandao upo chini sana nchini Nigeria, huwezi tuma pesa, vitu havikifanyika kwa mpangilio, hali hii inatumiza sisi raia katika taifa hili.”ameeleza Rome Williams.

00:13

Rome Williams, Raia wa Nigeria

Kwa upande wake Agbo Alex Arome, haungi mkono magavana wanaopinga, matumizi ya sarafu mpya, anasema hilo ndilo linalomfanya aunge mkono mabadiliko haya.

"Wanafunzi wamegoma kwa miezi, kuna uhaba wa mafuta, hatujaona kiongozi akitetea maslahi yetu, ila kile kinachowaathiri, wanaanza kulalamika…na kulaumu mahakama kuu, maana tumeona pale awali wanasiasa wenye pesa hutoa pesa hizo kwa raia wakati wa uchaguzi.”amesema Agbo Alex Arome.

00:15

Agbo Alex Arome, Raia wa Nigeria

Jumamosi hii raia wa Nigeria wanapiga kura kumchagua rais mpya baada ya muda wa rais buhari kukamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.