Pata taarifa kuu

WHO: Ugonjwa wa Kipindupindu waua zaidi ya 1,200 nchini Malawi

Ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea tangu Machi 2022 nchini Malawi umesababisha vifo vya watu 1,210 na karibu wagonjwa 36,950 wamerekodiwa, shirika la Afya Duiani, WHO, imesema Alhamisi, ikitoa wito wa "kuingilia kati" ili kuepusha kuzorota kwa hali ya mambo nchini Malawi.

Wagonjwa wa kipindupindu wanatibiwa katika CTC (Kituo cha Tiba ya Kipindupindu) wilayani Tete Machi 5, 2015. Mlipuko wa kipindupindu nchini Msumbiji ulianza mapema Februari kama sehemu ya matokeo ya mafuriko na hali mbaya ya usafi nchini. Tangu kuanza kwa milipuko ya kipindupindu kumekuwa na visa zaidi ya 3500 na karibu vifo 40 vimerekodiwa.
Wagonjwa wa kipindupindu wanatibiwa katika CTC (Kituo cha Tiba ya Kipindupindu) wilayani Tete Machi 5, 2015. Mlipuko wa kipindupindu nchini Msumbiji ulianza mapema Februari kama sehemu ya matokeo ya mafuriko na hali mbaya ya usafi nchini. Tangu kuanza kwa milipuko ya kipindupindu kumekuwa na visa zaidi ya 3500 na karibu vifo 40 vimerekodiwa. AFP - MAURICIO FERRETTI
Matangazo ya kibiashara

Kipindupindu kimeenea nchini Malawi tangu mwaka 1998, na milipuko wakati wa msimu wa mvua (mwezi Novemba hadi Mei), lakini janga la sasa limeenea hadi msimu wa kiangazi, kulingana na taarifa ya  magonjwa ya hivi punde ya Shirika la Afya Duniani.

Mlipuko huo ulitangazwa kuwa dharura ya afya ya umma na serikali ya Malawi mnamo Desemba 5. WHO inasaidia mamlaka, ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya matibabu na kusaidia kuongezwa kwa uwezo wa kupima.

Lakini "pamoja na ongezeko kubwa la kesi zilizoonekana katika mwezi uliopita, kuna hofu kwamba janga hilo litaendelea kuwa mbaya zaidi kwa kukosekana kwa hatua kali", imebaini WHO.

Shirika hilo linaona ni "haraka kuboresha upatikanaji wa maji ya kunywa na usafi wa mazingira". Moja ya sababu zinazochangia kiwango kikubwa cha vifo katika maeneo ya Mangochi, Blantyre, Machinga na Lilongwe ni kuchelewa kugunduliwa kwa wagonjwa kwani wagonjwa hufika kwenye vituo vya afya wakiwa wamechelewa, inasema WHO.

Shirika hilo linachukulia hatari ya ugonjwa huo kuenea kuwa "juu sana" katika ngazi za kitaifa na kikanda. Ugonjwa huu wa kipindupindu ndio mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa katika nchi hii maskini ya kusini mwa Afrika, ambayo ilikumbwa na vifo 968 mwaka 2001-2002, kulingana na WHO.

Kipindupindu huambukizwa kwa kumeza maji au chakula kilichochafuliwa na bakteria. Kwa kawaida husababisha kuhara na kutapika na inaweza kuwa hatari sana kwa watoto wadogo.

Takriban watu milioni tatu wamechanjwa (chanjo ya kumeza) hadi sasa. Lakini sehemu ya wakazi wa Malawi wanakataa matibabu kwa niaba la imani za kidini, jambo ambalo linachangia kuenea kwa ugonjwa huo.

Dunia inakabiliwa na kuzuka upya kwa ugonjwa wa kipindupindu, baada ya miaka mingi kupungua, ugonjwa unaotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Hivi sasa, nchi 23 zinakabiliwa na milipuko, na nchi zingine 20 zinazoshiriki mipaka ya ardhi na nchi zilizoathiriwa ziko hatarini, kulingana na WHO.

Hali hii inazuia upatikanaji wa chanjo, vipimo na matibabu. Ugonjwa huo unatishia zaidi ya watu bilioni moja duniani kote, mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema siku ya Jumatano.

WHO inakadiria hatari ya ugonjwa wa kipindupindu duniani kuwa "juu sana" kutokana na milipuko inayoendelea katika maeneo mengi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.