Pata taarifa kuu

Malawi: Ugonjwa wa kipindupindu waua watu zaidi ya 1,000

Ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea tangu mwezi Machi 2022 nchini Malawi umeua zaidi ya watu 1,000, Wizara ya Afya imetangaza hivi punde, ikilaumu ukosefu wa chanjo.

Wagonjwa wa kipindupindu wanatibiwa katika CTC (Kituo cha Tiba ya Kipindupindu) wilayani Tete Machi 5, 2015.
Wagonjwa wa kipindupindu wanatibiwa katika CTC (Kituo cha Tiba ya Kipindupindu) wilayani Tete Machi 5, 2015. AFP - MAURICIO FERRETTI
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo ilifikia 1,002 siku ya Jumanne, na kufanya mlipuko wa sasa wa kipindupindu kuwa mbaya zaidi katika rekodi katika nchi hiyo maskini ya kusini mwa Afrika, ambayo hapo awali ilishuhudia vifo 968 mnamo miaka ya 2001 na 2002, kulingana na Shirika la Afya Duiani (WHO).

Jumla ya watu 30,600 wameambukizwa tangu kesi za kwanza kuonekana mwaka jana. Kipindupindu huambukizwa kwa kunywa maji au kula chakula kilichoambukizwa na bakteria. Kwa kawaida husababisha kuhara na kutapika na inaweza kuwa hatari sana kwa watoto wadogo.

Kufikia mwezi Novemba, Malawi ilikuwa imepokea karibu dozi milioni tatu za chanjo ya kumeza kutoka kwa Umoja wa Mataifa. Lakini "tulitumia chanjo zote tulizokuwa nazo," msemaji wa wizara ya afya Adrian Chikumbe aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne.

"Ukweli kwamba kuna kampuni moja tu inayotengeneza chanjo ya kipindupindu duniani, na hali hii inafanya kuwa vigumu kupata dawa hiyo," ameongeza, kwani "tunashindania chanjo sawa na kila mtu". Sehemu ya wakazi wa Malawi pia wanakataa matibabu kwa kuzingatia imani za kidini, jambo ambalo linachangia kuenea kwa ugonjwa huo.

Mnamo mwezi Septemba, WHO iliripoti "kuongezeka" kwa idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kote ulimwenguni, baada ya kupungua kwa miaka kadhaa, na mabadiliko ya hali ya hewa yakiongeza sababu za kawaida kama vile umaskini na migogoro. Ugonjwa huu huathiri kati ya watu milioni 1.3 na milioni 4 duniani kila mwaka, na kusababisha vifo vya hadi watu 143,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.