Pata taarifa kuu
MALAWI- AFYA

Malawi yaomba msaada kabiliana na mlipuko wa kipindupindu

Mamlaka nchini Malawi imeomba msaada katika vita dhidi ya mlipuko  wa kipindupindu ambao kufikia wakati huu umesababisha vifo vya mamia ya raia katika taifa hilo.

Mlipuko wa Kipindupindu nchini Malawi
Mlipuko wa Kipindupindu nchini Malawi AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Serikali imeomba msaada wa vifaa vya matibabu, mchango wa vifa vya usafi katika maeneo ya shule ikiwemo msaada wa kifedha.

Malawi ilidhibitisha mlipuko wa kipindupindu mwezi machi mwaka wa 2022,maambukizi yakionekana kuongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni.

Hadi kufikia sasa, ungonjwa huo umesambaa karibu katika wilaya zote 28 nchini humo, hali inayozua hofu kwa raia.

Aidha tangazo hilo limeonekana kuzua mjadala katika mitandoa ya kijamii, wengi wakihoji ni kwa nini serikali inataka wafadhili  kufanya  mawasiliano kupitia anwani ya gmail badala ya barua pepe ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.