Pata taarifa kuu
MALAWI - KIPINDUPINDU

Ugongwa wa kipindupindu wawaua zaidi ya watu Elfu moja, Malawi

Shirika la afya duniani linasema watu 1,210 wamepoteza maisha nchini Malawi, kutokana na maambukizi ya kipindupindu tangu mwezi Machi mwaka uliopita.

Msumbiji iko katika hali ya tahadhari kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao tayari umeua watu katika nchi jirani ya Malawi.
Msumbiji iko katika hali ya tahadhari kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao tayari umeua watu katika nchi jirani ya Malawi. AFP - MAURICIO FERRETTI
Matangazo ya kibiashara

Mbali na vifo hivyo, Shirika hilo linasema watu wengine Elfu 37 wameambukizwa ugonjwa huo, wakati huu chanjo za kuzuia mlipuko huo, zikiwa haba, ikizingatiwa kuwa tangu mlipuko huo nchi ya Malawi, imefanya kampeni mbili kubwa za chanjo, lakini kutokana na uhaba wa vifaa, imetoa dozi moja tu kati ya dozi mbili zinazopendekezwa za chanjo ya kipindupindu.

Kwenye taarifa WHO inasema mlipuko wa ugonjwa huo, kwa sasa unashuhudiwa katika Wilaya 27 kati ya 29 za nchi hiyo na maambukizi yamekuwa yakiongezeka kwa kasi.

Kwa ongezeko kubwa la maambukizi katika mwezi uliopita, hofu ni kwamba mlipuko huo utaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo hatua hazitachukuliwa. Shirika hilo limeonya.

Mbali na Malawi, WHO inaonya kuwa ugonjwa huo huenda ukasambaa katika nchi jirani, wakati huu mataifa mengine zaidi ya 20 yakiwa katika hatari ya kuathiriwa na ugonjwa huo duniani.

Mwezi Januari mwaka huu, msemaji wa wizara ya afya ya Malawi aliliambia shirika la Habari la AFP kuwa mwishoni mwa mwaka 2022, walipokea takriban dozi milioni tatu lakini zote zimekwishatumika.

Mamilioni hatarini

WHO, imesema mbali na chanjo, juhudi zinaendelea za kuboresha usafi wa mazingira na upatikanaji wa maji safi, miongoni mwa juhudi zingine.

Maambukizi ya kipindupindu yameripotiwa katika mpaka wa Msumbiji.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, watu zaidi ya Bilioni moja kote duniani, wapo katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.