Pata taarifa kuu

WHO: Kuna hatari Uviko-19 kuibuka tena baada ya Afrika kushindwa kutumia chanjo kamili

Utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko-19, ambayo tayari iko kwenye kiwango cha chini ikilinganishwa duniani kote, unadorora barani Afrika, imebainisha Alhamisi ofisi ya kikanda ya Shirika la Afya Duniani (WHO), ambayo inahofia kwamba virusi hivyo vitachukua fursa hiyo kuibuka tena.

Muuguzi na mgonjwa wa Corona, wakiwa nyumbani nchini Kenya Julai 27 2021
Muuguzi na mgonjwa wa Corona, wakiwa nyumbani nchini Kenya Julai 27 2021 © Carol Korir
Matangazo ya kibiashara

Kufikia Oktoba 16, ni asilimia 24 pekee ya wakazi wa bara hilo ambao wamepatiwa chanjo kamili, ikilinganishwa na 64% duniani kote, imesema WHO barani Afrika katika taarifa iliyotolewa wakati wa mkutano wake wa kila wiki. Nchi tatu (Mauritius, Seychelles, Liberia) kati ya 54 zimefikia lengo la kimataifa lililowekwa na WHO la chanjo ya 70%, asilimia ambayo Rwanda pia iko kwenye hatu ya kufikiwa.

Katika bara hilo, utoaji wa chanjo umedorora katika kipindi cha miezi miwili iliyopita katika nusu ya nchi (27), "wakati idadi ya dozi zilizotolewa kila mwezi ilishuka kwa zaidi ya 50% kati ya mwezi Julai na Septemba", inabainisha WHO-Afrika. Mnamo mwezi Septemba, dozi milioni 23 za chanjo zilitumika, chini ya 18% mwezi Agosti, na chini ya 51% mwezi Julai, wakati dozi milioni 47 zilitolewa.

Idadi ya sindano zilizorekodiwa mwezi uliopita ni karibu theluthi moja ya kilele cha milioni 63 kilichofikiwa mnamo mwezi Februari 2022, taarifa hiyo imesema. Hata hivyo, WHO inasema imeona dalili za kuimarika mwezi Oktoba, huku dozi milioni 22 zikitolewa kufikia tarehe 16 mwezi huu, au asilimia 95 ya idadi iliyosimamiwa katika mwezi mzima wa Septemba.

"Mwisho wa janga la Uviko-19 unaweza kufikiwa, lakini maadamu Afrika inabaki nyuma sana duniani kufikia ulinzi kamili, kutakuwa na mwanya ambao virusi vinaweza kutumia ili kurejea kwa nguvu.", ameonya. Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa WHO barani Afrika. WHO inakumbusha kwamba ugumu wa kupata dozi ulipunguza kasi ya chanjo katika bara la Afrika mwaka 2021, lakini imeongeza kuwa matatizo haya sasa "yametatuliwa kwa kiasi kikubwa".

Kipaumbele, kulingana na WHO-Afrika, ni kulinda idadi ya watu walio hatarini zaidi. Kulingana na takwimu kutoka nchi 31, 40% ya wafanyakazi wa afya walikuwa wamechanjwa kikamilifu barani Afrika kufikia Oktoba 16. Katika kiwango cha kimataifa, WHO ilitangaza Jumatano huko Geneva kudumisha kiwango chake cha tahadhari katika mgogoro wa Uviko-19, ikionya juu ya janga ambalo "tayari limetushangaza na linaweza kuibuka tena".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.