Pata taarifa kuu

Wawili wafariki baada ya kupewa chanjo ya Johnson & Johnson Afrika Kusini

Mamlaka ya kusimamia dawa nchini Afrika Kusini, inasema watu wawili wamefariki dunia, baada ya kupata chanjo ya Johnson & Johnson ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UVIKO-19. 

Wafanyakazi wakishusha jeneza la mwathirika wa UVKO, kwenye makaburi huko Soweto, Afrika Kusini.
Wafanyakazi wakishusha jeneza la mwathirika wa UVKO, kwenye makaburi huko Soweto, Afrika Kusini. AFP - MICHELE SPATARI
Matangazo ya kibiashara

Mtu wa kwanza alipoteza maisha mwezi Agosti na mwingine, siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa uongozi wa mamlaka hiyo. 

Mamlaka hiyo imesema, imetoa taarufa kwa kampuni hiyo baada ya watu hao wawili waliopata chanjo hiyo, kupata changamoto za kiafya. 

Katika majibu yake, kampuni hiyo imesema kuna visa vichache vya Guillain-Barre Syndrome (GBS) ambayo huwapata baadhi ya watu waliopata chanjo hiyo ndani ya siku 42. 

Hata hivyo, imesema madhara hayo hayatokei mara kwa mara lakini haikusema iwapo visa vilivyoripotiwa ni kutoka nchini Afrika Kusini ambayo watu Milioni 9 wamepata chanjo hiyo. 

Afrika Kusini imesajili zaidi ya kesi Milioni 4 za Uviko 19 na vifo zaidi ya Laki Moja na Elfu mbili, ikiwa ndio nchi yenye idade kubwa ya maambukizi barani Afrika 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.