Pata taarifa kuu

Kiwanda cha kwanza cha chanjo ya Covid barani Afrika kutengenezwa Afrika Kusini

Afrika Kusini, ikiongoza mapambano ya upatikanaji sawa wa chanjo za Covid, imezindua kiwanda cha kwanza katika bara Afrika Jumatano huko Cape Town ambacho kitatengeneza dozi kutoka A hadi Z, kinachofadhiliwa na bilionea wa bayoteknolojia Patrick Soon-Shiong.

Rais Cyril Ramaphosa, kushoto, na mfanyabiashara Patrick Soon-Shiong wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kampuni ya kutengeneza dawa dhidi ya Covid, Afrika Kusini.
Rais Cyril Ramaphosa, kushoto, na mfanyabiashara Patrick Soon-Shiong wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kampuni ya kutengeneza dawa dhidi ya Covid, Afrika Kusini. GIANLUIGI GUERCIA POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Lengo ni kuzalisha "chanjo ya kizazi cha pili, na tunataka kuitengeneza barani Afrika, kwa ajili ya Afrika, na kuisafirisha duniani kote," amesema mfanyabiashara huyo kutoka Marekani mwenye asili ya China, ambaye alizaliwa Afrika Kusini. Chanjo za kwanza zitatolewa mwaka huu na lengo ni kufikia dozi bilioni moja kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.

"Leo tunathibitisha kwamba tunajitosheleza kama bara, na tunapaswa kujivunia kile tunachofikia," Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema.

Nchi ya Afrika iliyoathiriwa zaidi na virusi hivyo, ina zaidi ya kesi milioni 3.5 ikiwa ni pamoja na vifo 93,400, wakati bara la Afrika lilirekodi kesi zaidi ya milioni 10 mwezi Januari, kulingana na Umoja wa Afrika. Maambukizi yameongezeka tangu kirusi kipya aina ya Omicron kilipogunduliwa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.