Pata taarifa kuu

Afrika Kusini yarekodi ongezeko la visa vya maambukizi ya kirusi cha Omicron

Afrika Kusini inasema kirusi cha Omicron kilichogundulika nchini humo mwezi Novemba, kiwango cha maambukizi kimefika kiwango cha juu bila ya visa vipya kuongezeka lakini vifo hushudiwa.

Mfanyakazi wa huduma ya afya anapima Covid-19 PCR katika maabara ya Lancet huko Johannesburg, Novemba 30, 2021.
Mfanyakazi wa huduma ya afya anapima Covid-19 PCR katika maabara ya Lancet huko Johannesburg, Novemba 30, 2021. AFP - EMMANUEL CROSET
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imesababisha watalaam nchini humo kupendekeza kuondolewa kwa marufuku ya watu kutembea usiku, kwa mara ya Kwanza baada ya miezi 21. 

“Ni mtazamo wa watalaam kuwa kirusi cha  Omicron kimesambaa sana na kufika katika kiwango cha juu, na hatutarajii kitasambaa zaidi,  lakini pia hatujaona ongezeko la wagonjwa hospitalini, kwa hivyo basi tumefikia uamuzi huu, kwa sababu za kiuchumi na lengo letu ni kutumia kila njia kufungua uchumi, “ amesemaMondli Gungubele, Waziri katika Ofisi ya rais Cyril Ramaphosa.

Uamuzi huu wa Afrika Kusini unakuja wakati huu baadhi ya mataifa ya Afrika, yakichukua hatua za kupunguza kusambaa kwa kirusi hicho kinachosambaa kwa kasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.