Pata taarifa kuu
CONGO-JAMII

Covid-19 nchini Congo-Brazzaville: Sassou-Nguesso awekwa karantini

Rais wa Congo-Brazzaville Denis Sassou-Nguesso, 78, yuko karantini baada ya watu kadhaa wa karibu kuthibitishwa kuwa wana maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19. Rais Sasouu amelazimika kuahirisha ziara yake huko Pointe-Noire, mji mkuu wa kiuchumi wa Congo-Brazzaville

Denis Sassou-Nguesso, Rais wa Congo-Brazzaville.
Denis Sassou-Nguesso, Rais wa Congo-Brazzaville. AFP PHOTO / THIERRY CHARLIER
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais inasema, kulingana na itifaki za afya zinazotumika nchini Congo-Brazzaville, rais, akiwa ametangamana na mgonjwa wa Covid-19, anatakiwa kuzingatia muda wa kukaa karantini.

Muda wa kukaa karantini haujaainishwa na baraza la mawaziri, ambalo linasema kwamba watu kadhaa katika msafara wa karibu wa rais wa Jamhuri hivi karibuni wamepatikana na virusi vya Covid-19.

Baada ya uchunguzi, rais wa Jamhuri alipimwa lakini hakupatikana na virusi vya Corona, kulingana na taarifa hiyo.

Tangu Desemba 15 rais hajafanya ziara yoyote

Mara ya mwisho Denis Sassou-Nguesso kuonekana hadharani huko Brazzaville ilikuwa Jumatano (Desemba 15) wakati wa uzinduzi wa hospitali kuu katika sehemu ya kaskazini mwa mji wa Brazzaville. Lakini siku iliyofuata aliwakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Jean-Claude Gakosso, katika mkutano kati ya Uturuki na Afrika mjini Istanbul. Pia aliahirisha ziara iliyokuwa imepangwa kufanyika jana na hadi Jumanne huko Pointe-Noire (kusini).

Hivi majuzi Congo-Brazzaville ililegeza hatua kadhaa za kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, hasa kwa kuidhinisha kufanyika sherehe za harusi. Nchi hii tayari imerekodi takriban vifo 360 vilivyosababishwa na Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.