Pata taarifa kuu

Covid-19: Côte d'Ivoire yakabiliwa na ongezeko la idadi ya visa vya maambukizi

Nchini Côte d'Ivoire, karibu kesi 1,600 za maambukizi ya Covid-19 zilitambuliwa Alhamisi, Desemba 30 na mamlaka ya afya. Hii ni rekodi tangu kuanza kwa janga hili. Idadi ya maambukizi imekuwa ikiongezeka kwa siku chache zilizopita.

Mbele ya Kituo cha Hospitali ya Chuo Kikuu HUKO Treichville, Machi 12, 2020.
Mbele ya Kituo cha Hospitali ya Chuo Kikuu HUKO Treichville, Machi 12, 2020. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Kesi 1,578 zimetambuliwa. Hali ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini Côte d'Ivoire, ambayo imerekodi ongezeko kubwa la maambukizi ya Covid-19 kwa siku moja. Siku moja kabla, nchi ilikuwa tayari imevuka idadi ya kesi 1,502. Hata kama Wizara ya Afya haiwezi kutoa maelezo ya mlipuko huu au maelezo ya uwezekano wa kuwepo kwa Omicron nchini, wizara hiyo inahakikisha kwamba "hali ya majanga inadhibitiwa".

Sampuli 4,549 zilichukuliwa siku ya Alhamisi na 5,300 Jumatano, zaidi ya mara mbili ya sampuli za kawaida ambazo ni kati ya 2,000 na 2,500 zinachunguzwa kila siku. Hata hivyo, hata kama sampuli zaidi zilichunguzwa, kiwango cha maambukizi bado kiko juu: 34.7% ya maambukizi Alhamisi hii, Desemba 30 baada ya 28% siku iliyotangulia, Jumatano. Kiwango ambacho kimekuwa kikipanda sana kwa wiki moja.

Katika siku za hivi karibuni, serikali imeamua kupima abiria kutoka nchi zilizo hatarini kwenye uwanja wa ndege. Ili kufanya hivyo, pia iliagiza maabara za kibinafsi kuongeza uwezo wa uchunguzi wa sampuli.

Kufikia sasa, idadi ya vifo vinavyotokana na janga hilo haipandi sana. Nchini Côte d'Ivoire, watu 712 wamefariki kutokana na Covid-19 tangu virusi hivyo vilipozuka nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.