Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-USHIRIKIANO

Rais wa Afrika Kusini Ramaphosa aimarisha uhusiano na Ouattara

Rais wa Afrika Kusini anaendelea na ziara yake katikaukanda wa Afrika Magharibi. Tangu Desemba 1, Cyril Ramaphosa yuko nchini Côte d'Ivoire, katika ziara ya kwanza ya kiserikali mjini Abidjan tangu Nelson Mandela alipokuwa rais mwaka 1991. 

Marais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na raia wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Abidjan, Desemba 2, 2021.
Marais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na raia wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Abidjan, Desemba 2, 2021. REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi, Desemba 2, nchi hizo mbili zilitia saini mikataba tisa ya ushirikiano wa nchi mbili kwa lengo la ''kuongeza na kuimarisha biashara; pia ni nchi ambazo zina kauli moja kwenye mikutano ya kimataifa.

Dola nusu bilioni, ni kiasi cha biashara kati ya Afŕika Kusini na Côte d'Ivoire ambacho nchi hizo mbili zinataka kuongeza, hasa kwa mikataba ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika nyanja za ulinzi, kilimo au hidrokaboni.

Usawazishaji

Nchi hizo mbili zinataka kuongeza biashara zao, lakini pia pengine kusawazisha, kwa sababu leo, kama makampuni makubwa kama MTN au Standard Bank yanafanya kazi nchini Côte d'Ivoire, makampuni machache ya Côte d'Ivoire ndio pekee yanafanya kazi Afrika Kusini. Wakati huo huo rais Alassane Ouattara ametolewa wito kwa makampuni nchini humokufanya kazi nchini Afrika Kusini.

"Ujumbe ambao ningependa kutuma kwa zaidi ya yote kwa sekta binafsi nchini Côte d'Ivoire, ambayo itavutia zaidi soko la Afrika Kusini, labda soko la kwanza barani Afrika, lenye Pato la Taifa ambalo ni mara tano ya Pato la Taifa la Côte d'Ivoire, alisema rais wa Côte d'Ivoire. Kwa hivyo ningependa kampuni zetu za Côte d'Ivoire kuingia ubia nchini Afrika Kusini. "

Zaidi ya biashara, nchi hizo mbili pia zinakusudia kuimarisha uhusiano wao katika sekta ya kidiplomasia. Kila mwaka, watashauriana katika mikutano ya kawaida ili kuratibu misimamo yao kuhusu siasa za kimataifa. Mtafaruko uliibuka tangu Alhamisi wiki hii, hasa kuhusu suala tata la kupatikana kwa chanjo.

"Umoja"

"Mimi na wewe tunasalia na wasiwasi kwamba Afrika na mataifa mengine yanayoendelea yanaendelea kuhangaika na upatikanaji mdogo wa chanjo muhimu kuokoa maisha ya watu," alisema rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa. Serikali na washirika wa kimataifa lazima waungane kupata hakikisho la kimataifa ambalo linahakikisha kwamba chanjo na matibabu vinatolewa kwa kiwango kikubwa na kupatikana kwa wote, kwa uhuru na haki. "

Cyril Ramaphosa alitoa wito jana wa kuondolewa kwa marufuku ya kusafiri dhidi ya Afrika Kusini na nchi nyingine Kusini mwa Afrika kutokana na ugunduzi wa kirusi kipya cha Omicron kilichogunduliwa na wanasayansi wa Afrika Kusini. Kufungwa kwa mipaka kumesababisha athari kubwa kwa uchumi wa nchi yake, alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.