Pata taarifa kuu

Omicron ilikuepo Uholanzi tangu Novemba 19, kabla ya Afrika Kusini

Aina mpya ya kirusi cha Corona ya Omicron inasambaa na inatia wasiwasi ulimwengu. Mamlaka ya afya ya Uholanzi imetangaza Jumanne, Novemba 30 kwamba tayari walikuwa wamegundua kirusi hki kipya cha Omicron katika kipimo kilichochukuliwa Novemba 19. Sawa na takriban wiki moja kabla ya Afrika Kusini kutangaza kesi hiyo

Mabango kwenye barakoa za lazima na hitaji la kuheshimu hatua ya watu kuka umbali wa mita moja huko Nijmegen, mashariki mwa Uholanzi, Jumapili, Novemba 28, 2021.
Mabango kwenye barakoa za lazima na hitaji la kuheshimu hatua ya watu kuka umbali wa mita moja huko Nijmegen, mashariki mwa Uholanzi, Jumapili, Novemba 28, 2021. © AP Photo/Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

Kirusi kipya cha Omicron kiligunduliwa tayari katika sampuli mbili za majaribio zilizochukuliwa nchini Uholanzi Novemba 19 na 23, Taasisi ya Uholanzi ya Afya na Mazingira (RIVM) imesema Jumanne hii Novemba 30. Ukaguzi unaendelea ili kuona kirusi hiki kimesambaa kwa umbali gani.

Uholanzi iliripoti Jumatatu abiria 14 waliowasili kutoka Afrika Kusini wakiwa wameambukizwa kirusi kipya cha Omicron. Hata hivyo, sampuli hizo mbili zilichukuliwa hata kabla ya Pretoria kuripoti kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba iligundua aina mpya ya kitusi hiki Novemba 24, na kusababisha wimbi la hofu na mataifa mengi kupiga marufuku wasafiri kutoka kusini mwa Afrika.

Visa vingine vya kirusi kipya cha Omicron vimegunduliwa barani Ulaya katika sampuli zilizochukuliwa kabla hata Afrika Kusini haijatangazwa. Ubelgiji ilikuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kutambua kirusi kipya cha Omicron kwa mgonjwa "aliyeingia nchini humo kutoka nje ya nchi. Alipimwa na kupatikana na ameambukizwa kirusi hiki Novemba 22, "Waziri wa Afya wa Ubelgiji alibaini Novemba 26.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.