Pata taarifa kuu

Unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro: 'Mbinu ya vita, mateso na ugaidi', UN yalaani

Unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro "uliongezeka" mnamo mwaka 2023, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa siku ya Ijumaa.

Katika hospitali ya Panzi, huko Bukavu (Kivu Kusini), iliyoanzishwa na Dkt Mukwegue, waathiriwa wanatoka katika jamii zote.
Katika hospitali ya Panzi, huko Bukavu (Kivu Kusini), iliyoanzishwa na Dkt Mukwegue, waathiriwa wanatoka katika jamii zote. Sonia Rolley/RFI
Matangazo ya kibiashara

Ubakaji, utumwa wa ngono, ukahaba wa kulazimishwa, mimba za kulazimishwa, ndoa za kulazimishwa... ukatili huu unaendelea "kutumika kama mbinu ya vita, mateso na ugaidi", alitangaza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ambaye alipitisha mapitio ya hali nchini Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burma, Sudan, Mali na hata Haiti ambapo magenge yanafanya ukatili wa kingono dhidi ya wakazi wa vitongoji "hasimu", hasa wasichana wadogo ambao ni waathiriwa wa ubakaji wa magenge.

Waathiriwa "wengi" ni wanawake na wasichana, lakini "wanaume, wavulana na watu wa utambulisho wa jinsia tofauti pia wameathirika", na kesi nyingi zimeripotiwa katika maeneo ya kizuizini. "Mnamo mwaka wa 2023, pamoja na kuibuka kwa migogoro mipya na kuongezeka kwa migogoro iliyopo, raia wamekabiliwa na viwango vya juu vya unyanyasaji wa kijinsia unaohusiana na migogoro, ambao umezidishwa na athari za kuenea kwa silaha na kuongezeka kwa migogoro ya kijeshi," anabainisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu suala hili. Vurugu inayofanywa na makundi ya serikali au yasivyo ya serikali mara nyingi hutenda "bila kuadhibiwa kabisa".

Katika Afrika

Nchini Sudan, mwaka jana, Shirika la Afya Duniani lilikadiria kuwa karibu wanawake milioni 4 wa Sudan walikuwa katika hatari ya ukatili wa kijinsia. Ubakaji ni mkakati wa kijeshi, analaani Abrar Alaliem, daktari mjini Khartoum, akizungumza na mwandishi wetu wa kikanda, Gaëlle Laleix. "Ripoti za ubakaji zinaendelea Khartoum, Darfur na maeneo mengine mengi ya Sudan. Kutumia miili ya wanawake ndio kiini cha mkakati wao wa kuzua hofu, kuwasukuma watu kuondoka majumbani mwao, ili kutishia jamii. "

Wanawake wa Sudan wanapokea matibabu katika hospitali huko Adré, Chad, kwenye mpaka na Sudan.
Wanawake wa Sudan wanapokea matibabu katika hospitali huko Adré, Chad, kwenye mpaka na Sudan. © Mohaned Belal / AFP

Visa kama hivyo huripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo kwa miaka mingi, haswa Mashariki, wanawake wamekuwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia mikononi mwa wanamgambo, wanajeshi wa jeshi laserikali la Kongo au wanajeshi wa Burundi katika mkoa wa Kivu Kusini kama alivyoshtumu kwenye idhaa yetu mwezi Desemba mwaka uliyopita, Carina Tertsakian wa shirika lisilo la kiserikali la Haki za binadamu nchini Burundi (IDHB). Kazi iliyofanywa na Dkt Mukwege katika hospitali ya Panzi huko Bukavu, mashariki mwa DRC, na waathiriwa hawa, ilimletea Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo mwaka 2018.

Mashariki ya Kati katika uangalizi

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaelezea hasa "unyanyasaji wa kijinsia" uliofanywa na majeshi ya Israeli katika Ukingo wa Magharibi na "taarifa za kushawishi" juu ya ubakaji wa mateka waliochukuliwa Gaza na Hamas.

Kwa hivyo, katika Ukingo wa Magharibi, "taarifa zilizothibitishwa na Umoja wa Mataifa zilithibitisha ripoti kulingana na kwamba kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa wanawake na wanaume wa Kipalestina na vikosi vya usalama vya Israeli baada ya mashambulizi ya Oktoba 7 mara nyingi kuliambatana na kupigwa kwa kupita kiasi, dhuluma na udhalilishaji, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, kama vile kupigwa mateke sehemu za siri na vitisho vya ubakaji,” ripoti hiyo inasema. Pia unataja ripoti za vurugu "zinazofanana" zilizofanywa huko Gaza na vikosi vya Israeli baada ya kuanzishwa kwa mashambulizi ya ardhini.

Wanajeshi wa Israel katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Balata katika Ukingo wa Magharibi, Novemba 23, 2023.
Wanajeshi wa Israel katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Balata katika Ukingo wa Magharibi, Novemba 23, 2023. © AP - Majdi Mohammed

Kuhusu shutuma za unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa na Hamas wakati wa mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa mnamo Oktoba 7, unachukua hitimisho la mwakilishi wake maalum Pramila Patten iliyochapishwa mwanzoni mwa Machi baada ya ziara yake nchini Israeli. "Kuna sababu nzuri za kuamini kwamba unyanyasaji wa kijinsia" kama vile ubakaji na ubakaji wa wtu wengi ulifanyika angalau maeneo matatu mnamo Oktoba 7.

Kuhusu mateka waliochukuliwa na Hamas hadi Gaza, kuna "taarifa za wazi na zenye kushawishi" kwamba hasa ubakaji na mateso ya kingono "yalifanywa kwa wanawake na watoto wakati wa utekaji nyara". Na "sababu nzuri za kuamini kwamba vurugu kama hizo zinaweza kuendelea".

Katika muktadha huu, Katibu Mkuu anatoa wito kwa “suala la ukatili wa kijinsia unaohusiana na migogoro kuzingatiwa katika mikataba yote ya kisiasa na makubaliano ya kusitisha mapigano”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.