Pata taarifa kuu

Covid-19: Kesi tatu zakirusi kipya cha Omicron zagunduliwa nchini Nigeria

Kirusi kipya cha Omicron kimegunduliwa Afrika Magharibi. Visa vitatu vya aina mpya ya kirusi hiki kipya cha Covid-19 vimegunduliwa nchini Nigeria, kwa watu ambao walikuwa wamesafiri kwenda Afrika Kusini. Maafisa wa afya wanakiri kuwa kunaweza kuwa na kesi zaidi.

Mhudumu wa afya anafanya vipimo vya PCR huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria, Novemba 29, 2021.
Mhudumu wa afya anafanya vipimo vya PCR huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria, Novemba 29, 2021. AP - Gbemiga Olamikan
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa leo na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Nigeria. Ugunduzi ambao bila shaka ulikuwa kiini cha majadiliano Jumatano hii asubuhi kati ya rais Muhammadu Buhari na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ziarani Abuja.

"Sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa vipimo vilivyoombwa kutoka kwa wasafiri wote siku mbili baada ya kuwasili kwao Nigeria zimepatikana na kirusi kipya cha Omicron kwa watu watatu ambao hapo awali walisafiri kwenda Afrika Kusini," kilisema Kituo cha Kudhibiti Magonjwa.

Watu hawa waliowasili nchini Nigeria wiki jana wamewekwa karantini. Wanafuatiliwa na msako wa watu waliotangamana nao unaendelea lakini mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Nigeria anakiri, "si swali tena kama kuna visa vingine vya kirusi kipya nchini, lakini ni kujuwa ni wakati gani vitagunduliwa”.

Ghana, jirani yake wa Afrika Magharibi, pia imetangaza Jumatano kwamba imegundua kesi za kirusi cha Omicron kwaa wasafiri kutoka Nigeria na Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.