Pata taarifa kuu

Rais wa Afrika Kusini ataka marufuku ya usafiri kuondolewa dhidi ya nchi yake

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amelaani hatua ya mataifa mbalimbali duniani, kuamua kusitisha safari za ndege kutoka nchini mwake nan chi jirani baada ya kugundulika kwa kirusi kipya cha Covid 19 kilichopewa jina Omicron wiki iliyopita.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosaalaani marufuku ya usafiri dhidi ya nchi yake.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosaalaani marufuku ya usafiri dhidi ya nchi yake. Sumaya HISHAM POOL/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Ramaphosa amesema amesikitishwa na hatua ya mataifa hayo ambayo ni pamoja na Marekani, yale ya Umoja wa Ulaya na Uingereza, na kusisitiza kuwa kitendo hicho hakikustahili kufanyika na kutaka uamuzi huo kubadilishwa haraka iwezekanavyo.

Shirika la afya duniani linasema, kirusi hicho kipya ndio chanzo cha kusambaa kwa maambukizi makubwa katika mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo WHO nayo inaonya dhidi ya uamuzi wa mataifa malimbali kuzuia safarai za ndege na kuchukua hatua nyingne, kwa kile inachosema hatua za kisayansi ndizo zinazopaswa kuchukuliwa.

Aidha, watalaam wa Shrika hilo la afya, wanasema itachukua wiki kadhaa kubaini undani ya kirusi hiki ambacho kimezua wasiwasi duniani.

Mpaka sasa kirusi hicho cha Omicron kimeripotiwa nchini Uingereza, Ujerumani, Australia na Israeli ambayo imetanagza kufunga mipaka yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.