Pata taarifa kuu

Nchi mbalimbali zachukuwa hatua kali dhidi ya aina mpya ya kirusi B.1.1.529

Mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Ufaransa yameanza kuzuia safari za ndege kutoka mataifa ya Kusini mwa bara la Afrika, baada ya aina mpya ya kirusi cha Covid 19  kilichopewa jina la B.1.1.529  kugunduliwa mapema wiki hii, huku Ubelgiji ikiripoti kisa cha kwanza cha kirusi hicho.

Madaktari wakimhamisha mgonjwa wa Covid-19 kwenye ndege ya kusafirisha vifa vya matibabu katika Uwanja wa Ndege wa Memmingen, Bavaria;
Madaktari wakimhamisha mgonjwa wa Covid-19 kwenye ndege ya kusafirisha vifa vya matibabu katika Uwanja wa Ndege wa Memmingen, Bavaria; CHRISTOF STACHE AFP
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa  imesema inasitisha safari hizo kwa kipindi cha saa 48 zijazo, huku Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen akipendekeza hatua zaidi kuchukuliwa kuhusu safari za ndege kutoka Kusini mwa Afrika.

Uingereza nayo imechukua hatua kama hii, na kusitisha safri za ndege kutoka mataifa ya Afrika Kusini, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji, Namibia na Eswatini.

Kenya nayo imetangaza kuwa abiria kutoka mataifa hayo, watawekwa karatini na kufanyiwa vipimo mara kadhaa kabla ya kuruhusiwa kutanagamana na watu nchini humo.

Wanasayansi wanasema wanaendelea kufanya utafiti zaidi kuhusu kirusi hiki kipya, ambacho kinaonekana kuzua wasiwasi mkubwa, huku biashara katika masoko ya hisa duniani, ikiyumba.

Shirika la afya duniani WHO wanakutana siku ya Ijumaa, kujadilli aina hii mpya ya kirusi na kukipa jina la Kigiriki kama lilivyo kwa kirusi cha Alpha na Delta.

Mpaka sasa, Shirika la afya duniani linasema hata hivyo ni visa chini ya 100 ya kirusi hiki kipya ndivyo vilivyoripotiwa katika mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini, visa vinne nchini Botswana na kimoja huko Hong Kong.

Hii inajiri wakati huu Afrika Kusini, asilimia 24 ya watu wake wakiwa wamepokea chanjo kamili ya kupambana na Covod-19, na kuna hofu kuwa, huenda kirusi hiki kipya kikasambaa kwa kasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.