Pata taarifa kuu
MOROCCO-USHIRIKIANO

Covid-19: Morocco yasitisha safari za ndege na Ufaransa

Morocco imeamua kusitisha safari za ndege za mara kwa mara kwenda na kutoka Ufaransa, huku hali ya kiafya ikizidi kuzorota tena nchini Ufaransa.

Ndege ya shirika la ndege la Royal Air Maroc kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mohammed V huko Casablanca. (picha ya kumbukumbu)
Ndege ya shirika la ndege la Royal Air Maroc kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mohammed V huko Casablanca. (picha ya kumbukumbu) Maher27777/CC/Wikimédia Commons
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linakuja saa chache baada ya kuimarishwa kwa hatua za afya nchini Ufaransa.

"Mamlaka ya Morocco imeamua kuahirisha hatua ya kusitishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka na kwenda Ufaransa hadi Jumapili 28 saa 11:59 usiku. badala ya Ijumaa Novemba 26 2021," Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Ufaransa, mshirika wake wa kwanza wa kiuchumi, inakabiliwa na wimbi la tano la Covid, wakati Morocco, badala yake, imejikuta hali ya ugonjwa huo ikiboresha sana, hali ambayo iliwezesha viongozi wa Morocco kuondoa amri ya kutotoka nje usiku ambayo ilikuwa imedumu kwa miezi kadhaa.

Kwa wiki kadhaa, Morocco ilikuwa imeimarisha udhibiti wake kwa wasafiri kutoka Ulaya, Algeria na Tunisia.

Mwezi uliopita, viongozi wa Morocco pia walisitisha safari za ndege kwenda na kutoka Ujerumani, Uholanzi, Uingereza na Urusi, kwa sababu ya hali ya kiafya inayoendelea katika nchi hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.