Pata taarifa kuu

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex aambukizwa virusi vya Corona

Jean Castex amepatikana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 Jumatatu jioni, Novemba 22, halia ambayo ilimlazimu mwenzake wa Ubelgiji Alexander De Croo na mawaziri wake wanne kujiweka karantini.

Jean Castex Oktoba 26, 2021 katika Bunge.
Jean Castex Oktoba 26, 2021 katika Bunge. Geoffroy van der Hasselt AFP
Matangazo ya kibiashara

Jean Castex atajitenga kwa kipindi cha kumi na ratiba yake itarekebishwa ili kumruhusu kuendelea na shughuli zake, ofisi ya waziri mkuu, Matignon, ilisema Jumatatu jioni. Waziri Mkuu aliumwa Jumatatu jioni na kupatikana na "dalili kidogo", kulingana na wasaidizi wake, hasa "kikohozi".

Jean Castex alikwenda Brussels siku ya Jumatatu asubuhi ambapo alikutana na mwenzake Alexander de Croo na mawaziri wake wengine wanne kwa mkutano kuhusu suala la usalama. Aliporejea, alifanya uvipimo vya PCR kwa sababu alikuwa amefahamishwa kwamba mmoja wa binti zake mwenye umri wa miaka 11 alikuwa amepimwa na kukutwa na Covid-19, amesema Valérie Gas, mwandishi wa habari katika kitengo cha siasa cha RFI. "Alifanya uchunguzi wa PCR mara moja, ambao ulibainisha kuwa ameambukizwa virusi vya Corona," Matignon alisema.

Kwa tahadhari na hata kabla ya kupata matokeo ya vipimo vyake, Waziri Mkuu pia alikuwa ameongoza mkutano uliopangwa kufanyika Jumatatu jioni na viongozi waliochaguliwa wa Guadeloupe kwa njia ya video kutoka ofisi yake ili kuepuka kuwasiliana nao. Wakati huo Jean Castex hakuonekana na dalili zozote.

Waziri Mkuu alikuwa ameandamana na Mawaziri wa Vikosi vya Jeshi Florence Parly, wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin, wa Sheria Éric Dupond-Moretti na Waziri wa Mambo ya Ulaya Clément Beaune. Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Ndani Nicolas Lerner, yule wa Usalama wa Nje Bernard Emie, Mwendesha Mashtaka mkuu anayehusika na Kupambana na Ugaidi Jean-François Ricard na Mratibu wa Kitaifa wa Ujasusi na Mapambano dhidi ya Ugaidi Laurent Nunez pia walikuwa sehemu ya ujumbe wakati wa mkutano huu.

Waziri Mkuu alikuwa tayari ametangamana na binti yake aliyeambukizwa virusi vya Corona, lakini hadiwakati huo alikuwa hajaambukizwa virusi hivyo. Takriban mwaka mmoja baada ya Emmanuel Macron kupatikana na virusi hivyo, waziri wake mkuu pia anapatikana na virusi vya Corona wakati ana chanjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.