Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFYA

Ufaransa: Maandamano mapya yazuka kupinga sheria dhidi ya Corona

Nchini Ufaransa, wapinzani wa sheria dhidi ya Corona na chanjo ya lazima kwa wahudumu wa afya wameandamana tena Jumamosi hii, Agosti 7, 2021, kwa wikendi ya nne katika jiji kuu la nchi hiyo Paris na katika miji zaidi ya mia moja.

Maandamano mapya dhidi ya sheria ya Corona, Jumamosi Agosti 7 huko Paris.
Maandamano mapya dhidi ya sheria ya Corona, Jumamosi Agosti 7 huko Paris. Stephane de Sakutin AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutoka Toulon hadi Lille, watu kutoka tabaka mbalimbali wameandamana Jumamosi hii. Wizara ya Mambo ya Ndani ilibaini kamba waandamanaji 204,000 waliandamana Julai 31. "Tunatarajia idadi kama hiyo ya waandamanaji" wikendi hii, kimetabiri chanzo cha polisi, maandamano yalipangwa kufanyika katika zaidi ya miji 150.

Hivi karibuni serikali ilitangaza kibali kipya cha afya cha virusi vya Corona kinachohitajika ili kuingia mgahawani au kusafiri kwenye treni za kutoka mji mmoja hadi mwingine.

Maandamano ya leo yamekuja ikiwa ni siku mbili kabla ya sheria hizo mpya kuanza kutekelezwa. Sheria hizo zinazoungwa mkono na Rais Emmanuel Macron zinahitaji ama kibali cha dozi kamili ya chanjo ya Covid-19, kuwa na umiliki wa cheti kinachoonesha mhusika hana mambukizi au kapona katika siku za karibuni kutokana na virusi hivyo ili kufurahia shughuli za kawaida za nje.

Rais Macron na serikali yake wana imani kwamba sheria hizo mpya zitawahimizaΒ Wafaransa wote kuchanjwa dhidi ya Covid-19 na kukiangamiza aina ya kirusi kipya kinachosambaa kwa kasi cha Delta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.