Covid-19: Kisiwa cha Reunion chawekwa chini ya masharti ya watu kutotoka nje
Kuanzia wikendi hii na kwa muda wa wiki mbili, Visiwa vya Reunion vitakuwa chini ya masharti ya watu kutotembea mchana na sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa kuanzia saa 12 jioni hadi saa 11 Alfajiri.
Imechapishwa:
Kulingana na mkuu wa mkoa, maeneo kadhaa ya mji huo yanakabiliwa na "ongezeko lisilo kuwa la kawaida ya maambukizi ya visa vya Corona".
Hii ni mara ya kwanza tangu kutangazwa kwa hatua za watu kutotembea katika msimu wa majira ya Joto 2020. Kutokana na kuongezeka kwa kesi za Covid-19, Visiwa vya Reunion vimewekwa chini ya masharti ya watu kutotembea mchana, "kumetangzwa sheria ya kutotoka nje usiku kuanzia saa 12 jioni hadi saa 11 Alfajiri", hatua ambazo zitaanza kutekelezwa wikendi hii "kwa kipindi cha wiki mbili ", mkuu wa mkoa wa Reunion, Jacques Billant ametangaza Alhamisi jioni Julai 29.
Jacques Billant ametangaza pia kwamba mikahawa, baa na kumbi za michezo vitafungwa katika kipindi chote hicho cha wiki mbili.
Confinement |
— Préfet de La Réunion (@Prefet974) July 29, 2021
📍 Dans un rayon de 10 km autour du domicile du lundi au samedi
📍 Dans un rayon des 5km autour du domicile le dimanche
⚠ Dérogations pour les déplacements de +10 km UNIQUEMENT sur présentation d'une attestation et d'un justificatif
👉 https://t.co/MIIHwXyU5c pic.twitter.com/CLhkKjtrrc
Guadeloupe na Martinique zakabiliwa na ongezeko la maambukizi
Hatua hizi pia zitatekelezwa katika maeneo ya Antilles ya Ufaransa kama "Gaudeloupe na Martinique" ambapo kunaripotiwa ongezeko la visa vya maambukizi. Katika maeneo haya 17% tu ya raia ndio wamepewa chanjo wakati nchini Ufaransa 50% ya raia wamechanjwa.