Pata taarifa kuu
AFRIKA

COVID-19: Ufaransa kutoa dozi Milioni 10 za chanjo kwa nchi za Afrika

Ufaransa, imetangaza kuwa itatoa Dozi Milioni 10 za chanjo ya AstraZeneca na Pfizer kwa mataifa ya bara Afrika kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo, kusaidia kulikabili janga la COVID-19.

Wahudumu wa afya wakisubiri wagonjwa wakati wa kampeni ya kutoa chanjo katika mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vy Corona huko Lenasia, Afrika Kusini, Aprili 21, 2020.
Wahudumu wa afya wakisubiri wagonjwa wakati wa kampeni ya kutoa chanjo katika mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vy Corona huko Lenasia, Afrika Kusini, Aprili 21, 2020. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa na Ofisi ya rais Emmanuel Macron siku ya Jumatatu, na kusema chanjo hizo zitapelekwa na kugawanywa kupitia Jukwa la Kimataifa la Covax na lile la Umoja wa Afrika AVAT.

Macron amesema kulishinda janga la Corona kunahitaji ushirikiano wa kila mmoja na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana na Umoja wa Afrika.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kuyashtumu mataifa tajiri duniani kujilimbikizia chanjo na kuyaacha yale masikini hasa ya bara Afrika, amepongeza hatua ya rais Macron na kusema msaada huo umekuja wakati mwafaka.

Aidha, Ufaransa inasema chanjo za kutosha zimenunuliwa kupitia Jukwaa la Umoja wa Afrika, AVAT ili kuwachanja watu Milioni 400 barani Afrika ifikapo mwezi Septemba.

Mpaka sasa, Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema ni watu Milioni 24 ndio waliopokea chanjo kamili ya COVID-19 ambayo ni sawa na asilimia 1.7 ya idadi ya watu barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.