Pata taarifa kuu
SENEGAL

Senegal: Sababu za kuongezeka kwa kasi kwa visa vya Covid-19

Visa vya Covid-19 vimeongezeka mara tisa nchini Senegal, kati ya miezi ya Juni na Julai. Mlipuko wa tatu ambao umeongezeka zaidi tangu Mei 17, na hivyo kusababisha kuongezeka kwa kasi kwa visa vya maambukizi na vifo. Alioune Badara Ly ametueuliwa kuwa mkurugenzi mpya wa kituo cha shughuli za dharura za kiafya cha Wizara ya Afya. Anaelezea ni kwanini Senegal inakabiliwa na wimbi jipya ambalo halijawahi kutokea nchini humo.

hudumu wa afya akimfanyia vipimo abiria kwenye basi huko Dakar (picha ya kumbukumbu).
hudumu wa afya akimfanyia vipimo abiria kwenye basi huko Dakar (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

"Sababu ya kwanza inahusiana na aina mpya ya kirusi cha Corona, Delta, kinayoambukia haraka," anasema Alioune Badara Ly. Ongezeko hili la idadi ya visa vya maambukizi iliambatana na wakati ambapo taasisi ya Pasteur ilionyesha kuwa kwa sampuli ambazo zilikuwa zikifuatiliwa, karibu 60% ilikuwa kirusi kipya aina ya Delta, kwa hivyo kulikuwepo na urahisi wa maambukizi kuweza kuongezeka zaidi. Sababu ya pili ni kwamba masharti ya kudhibiti Corona hayakutekelezwa kwa muda fulani raia.

Jambo la tatu ni kwamba pia tuliona mikusanyiko mingi, katika wiki iliyofuata sikuu kuu ya kuchinja kwa Waislamu (Tabaski), katika nkaribu mikoa yote, idadi ya kesi za jumla ziliongezeka kwa sababu iliendana na wakati, wakati kulikuwa na safari nyingi, ambapo wakaazi wa mji wa Dakar waliisafiri kwenda mikoani. Dakar, ambayo ni kitovu cha ugonjwa huo, ilikuwa na zaidi ya 65% ya kesi za maambukizi.

Lazima tuendelee kufanya kazi na kuhakikisha kuwa mikusanyiko imepigwa marufuku. Baadhi wamepigwa marufuku na magavana. Bado kuna hatua za kuchukuliwa, juhudi za kufanywa, "amebaini mkurugenzi mpya wa kituo cha shughuli za dharura za kiafya cha Wizara ya Afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.