Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFYA

Ufaransa yaonya kuhusu maambukizi zaidi katika visiwa vya Carribean

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema maambukizi makubwa ya virusi vya Covid-19 yanayoshuhudiwa kwenye visiwa inavyotawala hasa vya Carribean, ni kutokana na kiwango kidogo cha utoaji wa chanjo katika maeneo hayo.

Mhudumu wa afya kwenye mlango wa kituo cha afya huko Cayenne, Guyana, Juni 2020.
Mhudumu wa afya kwenye mlango wa kituo cha afya huko Cayenne, Guyana, Juni 2020. AFP - JODY AMIET
Matangazo ya kibiashara

Visiwa vilivyoathiriwa zaidi ni Martinique na  Guadeloupe. Waziri wa afya nchini Ufaransa Olivier Veran, anaonya kuwa kuna hatari ya maeneo ya bara pia kushuhudia maambukizi kama hayo.

Virusi vya Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS).

Virusi vipya vya Corona (COVID-19) viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Hivi ni virusi vipya vya korona ambavyo havijatambuliwa hapo awali kwa binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.