Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-USHIRIKIANO

Afrika Kusini yahisi kuadhibiwa baada ya ugunduzi wake kuhusu virusi vya Omicron

Ugunduzi wa uwepo wa aina mpya ya kirusi cha Corona umesababisha wimbi la mshtuko duniani kote. Kirusi hiki kimepewa jina la "Omicron" na Shirika la Afya Duniani na kuchukuliwa kuwa chanzo cha wasiwasi.

Mhudumu wa afya amevaa barakoa huko Soweto, Afrika Kusini, Novemba 26, 2021.
Mhudumu wa afya amevaa barakoa huko Soweto, Afrika Kusini, Novemba 26, 2021. REUTERS - SIPHIWE SIBEKO
Matangazo ya kibiashara

Takriban visa 100 vimetambuliwa nchini Afrika Kusini, lakini chimbuko lake ke bado halijajulikana. Hata hivyo nchi mbalimbali duniani  zinafunga mipaka yao dhidi ya Afrika Kusini na nchi kadhaa za kusini mwa Afrika. Afrika Kusini inahisi kuwa imetengwa baada ya kutangaza ugunduzi wake

"Tunaadhibiwa kwa kuwa wa wazi": hii ni kauli iliyotolewa na Profesa Tulio de Oliveria, mmoja wa watafiti waliofanya ugunduzi wa aina mpya ya kirusi cha Corona,  Omicron. Kufungwa kwa mipaka ya nchi za kigeni kunafadhaisha mamlaka ya Afrika Kusini, ameipoti mwandishi wetu wa Johannesburg, Romain Chanson.

Baadhi ya majibu na hatua "hazifai" amejibu Waziri wa Afya akinyooshea kidole nchi za Ulaya na Uingereza. "Tunahitaji kufanya kazi pamoja badala ya kuadhibu," Waziri Joe Phaahla amesema akionya dhidi ya kuibebesha Afrika Kusini mzigo wa lawama kuliko ktafuta pamoja ufumbuzi.

Ingawa haiwezekani kusema ni lini aina hii mpya ya kirusi ilionekana kwa mara ya kwanza, nchini Afrika Kusini ndiko ambako inaenea kwa kasi. Idadi ya visa vya maambukizo ya kirusi kipya inaongezeka katika karibu majimbo yote ya Afrika Kusini kulingana na Shirika la Afya Duniani. Kirusi hiki kinaambatana na kuanza kwa wimbi la nne la janga, ambalo uwezo wake unapaswa kufuatiliwa na nchi zote ulimwenguni.

Si haki, na ni uzembe wa nchi za nje kufunga mipaka yao na Afrika Kusini kwa kigezo cha ugunduzi ambao tunashirikiana na ulimwengu, hatupaswi kunyanyapaliwa.

Wakati huo huo sekta ya utalii, ambayo inachangia zaidi ya 8% ya Pato la Taifa, inahofia mgogoro mkubwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.