Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini yalegeza masharti ya kudhibiti Covid-19

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza kulegeza zaidi masharti ya kupambana na maambukizi ya Covid-19 baada ya  kuonekana kuwa maambukizi yameanza kupungua.

Hivi karibuni rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitangaza nia yake ya kuanza kutumika kwa "Hati ya kusafiri ya Covid-19 ", huku wengi wakipuuzia kuchanjwa dhidi ya Covid-19, katika nchi hii iliyoathiriwa zaidi na virusi vya Corona barani Afrika.
Hivi karibuni rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitangaza nia yake ya kuanza kutumika kwa "Hati ya kusafiri ya Covid-19 ", huku wengi wakipuuzia kuchanjwa dhidi ya Covid-19, katika nchi hii iliyoathiriwa zaidi na virusi vya Corona barani Afrika. Phill Magakoe / AFP
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Ramaphosa ameitaka Uingereza kuondoa masharti dhidi ya raia wake wanaokwenda katika taifa hilo la bara Ulaya.

Baraza la Mawari limeamua kuiondoa Afrika Kusini kutoka masharti ya kiwango cha pili mpaka kiwango cha kwanza kuanzia Oktoba tarehe moja, muda watu kutotembea sasa ni kati ya saa sita usiku mpaka saa 10 Alfajiri. Maeneo ya burudani kama hoteli sasa yatafungwa kuanzia saa tano usiku lakini uvaaji wa barakoa ni lazima kwenye maeneo ya umma

.

Hivi karibuni rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitangaza nia yake ya kuanza kutumika kwa "Hati ya kusafiri ya Covid-19 ", huku wengi wakipuuzia kuchanjwa dhidi ya Covid-19, katika nchi hii iliyoathiriwa zaidi na virusi vya Corona barani Afrika.

Katika hotuba kwa taifa kwa njia ya televisheni Jumapili Septemba 12, rais Cyril Ramaphosa alihakikisha kuwa chanjo kwa watu wazima ilikuwa sharti la lazima kufungua tena uchumi na kuepusha mlipuko wa nne wa maambukizi, wakati idadi ya kesi za maambukizi zilipungua kwa kiwango kikubwa nchini Afrika Kusini.

Katika wiki mbili, "tutatoa habari zaidi juu ya mfumo wa hati ya kusafiri ya chanjo ambayo inaweza kutumika kama uthibitisho wa chanjo kwa madhumuni mbalimbali na katika hafla mbalimbali," Cyril Ramaphosa alisema bila kutoa maelezo zaidi. Aliongeza kuwa "kushuka kwa visa vya maambukizi [...] kwa wiki chache zilizopita" itawezesha, hata hivyo, kulegeza hatua za kudhibiti virusi vya Corona kuanzia Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.