Pata taarifa kuu

Wanasayansi wachunguza kirusi aina ya C.1.2

Wanasayansi wanachunguza aina mpya ya kirusi kinachosabisha ugonjwa wa Covid-19, kilichobainika nchini Afrika Kusini. Kirusi hicho  kilichopewa jina la C.1.2, kiligunguliwa nchini Afrika Kusini mwezi Mei, lakini mpaka sasa Wanasayansi wanasema hakijaonesha uwezo wa kusambaa kwa kasi.

COVID-19 imesababisha vifo vingi duniani.
COVID-19 imesababisha vifo vingi duniani. © DR
Matangazo ya kibiashara

Tangu kugungulika kwake, kimesambaa kwenye mataifa saba barani Afrika, pamoja na nchi kadhaa za bara Asia, Ulaya na eneo la Asia-Pacific.

Wanasayansi wanasema wanachunguza kirusi hicho namna kinavyobadilika baada ya kuwekewa kinga za mwili.

Hata hivyo, mtalaalam wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Maria van Kerkhove, amesema kirusi hicho hakionekani kusambaa kwa kasi kama ambavyo ilikuwa inahofiwa.

Mpaka sasa kirusi aina ya Delta ndio maarufu nchini Afrika Kusini na duniani, na WHO inasema iwapo kutakuwa na kirusi kingine, itatangaza.

Tangu kuzuka kwa janga la Covid-19, Afrika Kusini imeripoti maambukizi 2,770,575 na vifo zaidi ya Elfu 81.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.