Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-USHIRIKIANO

Covid: Aina mpya ya kirusi cha Omicron chazua hofu duniani

Kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha corona nchini Afrika Kusini kumezua hofu duniani kote katika siku za hivi karibuni. Baadhi ya nchi, hasa barani Ulaya, zimetangaza kuimarishwa kwa hatua za kupambana na janga la Covid.

Kikao cha kwanza kiimarishwa kutokana na aina mpya ya kirusi cha corona cha Omicron: mkutano wa mawaziri wa Shirika la Biashara Ulimwenguni uliopangwa kufanyika Geneva kuanzia Jumatatu.
Kikao cha kwanza kiimarishwa kutokana na aina mpya ya kirusi cha corona cha Omicron: mkutano wa mawaziri wa Shirika la Biashara Ulimwenguni uliopangwa kufanyika Geneva kuanzia Jumatatu. © Fabrice COFFRINI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la afya ulimwenguni WHO limekitangaza kirusi kipya cha B.1.1.529, kilichogundulika hivi karibuni nchini Afrika Kusini kuwa chenye kutia wasiwasi na kukiita jina la Omicron.

Omicron, aina mpya ya kirusi hiki iliyochukuliwa kuwa ya kutisha na Shirika la Afya Duniani, imesababisha kuanguka kwa vituo vya kifedha kote ulimwenguni.

Bei ya mafuta haijaepuka hali hii na sasa ulimwengu mzima unajitayarisha kukabiliana na ujio wa aina hii ya kirusi ambayo inaweza kudhibitisha kuwa ya kuambukiza na labda sugu zaidi kuliko aina ya kirusi cha Delta.

Nchi kadhaa duniani sasa zimeamua kuweka marufuku au kuweka masharti ya usafiri ya kutoka au kuelekea nchini Afrika Kusini.

Wasafiri kutoka Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe, Lesotho na Eswatini hawataweza kuingia nchini Uingereza isipokuwa kama watakuwa ni raia wa Uingereza na Ireland au wakazi wa Uingereza.

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa safari za kutoka Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Namibia, Lesotho, Eswatini, Msumbiji na Malawi zitazuiwa, uamuazi huu ukiwa ni sawa na ule uliochukuliwa awali na Muungano wa Ulaya (EU). Hatua hii itaanza kutekelezwa kuanzia Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.