Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini kukarabati vilivyoharibiwa katika ghasia za hivi karibuni

Machafuko nchini Afrika Kusini ya Julai mwaka jana yalisababisha athari kubwa na ambazo itakuwa si rahisi kukarabati vilivyoharibiwa katika ghasia hizo. Miongoni mwa athari zingine, uharibifu ambao utagharimu sana Afrika Kusini, wakati nchi hiyo inakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi kutokana na janga la Corona.

Ghala likiteketea kwa moto huko Durban, Julai 14, 2021.
Ghala likiteketea kwa moto huko Durban, Julai 14, 2021. REUTERS - ROGAN WARD
Matangazo ya kibiashara

Mgogoro huu, mkubwa zaidi nchini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, ulizuka kufuatia kufungwa kwa rais wa zamani Jacob Zuma kwa kudharau mahakama, na uliendelea kushika kasi kadri siku zilivyokwenda, ukichochewa na umaskini na ukosefu wa usawa. Watu zaidi 350 waliuawa katika ghasia hizo.

Ghasia hizo pia zilisababisha uharibifu mkubwa na athari kubwa za kiuchumi, kwani vituo vya ununuzi na maghala yaliporwa, katika maeneo karibu na Durban na Johannesburg.

Kulingana na Sasria, kampuni ya bima ya umma inayoshughulikia kesi za fidia kufuatia ghasia hizo, uharibifu unaweza kufikia euro bilioni 1.5, kufuatia uharibifu na visa vya uporaji katika vituo 200 vya kibiashara na maduka 3,000. Kampuni hiyo inayomilikiwa na serikali inachukulia hii kuwa machafuko yaliyosababisha hasara kubwa zaidi duniani katika muongo mmoja uliopita.

Athari kwa uchumi inaweza kuwa kubwa zaidi, kwani shughuli zilizorota kwa wiki nzima nchini kote wakati vurugu hizo zilipozuka., huku malori yakichomwa moto na barabara kuu zinazounganisha mkoa wa kusini na bandari ya Durban kufngwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.