Pata taarifa kuu

Covid-19: Kesi ya kwanza ya kirusi kipya cha Corona yagunduliwa nchini Ubelgiji

Timu ya wanasayansi wa Afrika Kusini ilitangaza Alhamisi, Novemba 25, ugunduzi wa aina mpya ya Covid-19. kirusi hiki kilipewa jina kwa Kigiriki "Mu". Inachukuliwa kuwa ni kirusi ambacho kinatia "wasiwasi" kwa sababu kinaambukia kwa haraka, ingawa kesi chache zimetambuliwa kwa sasa. Kesi moja imetambuliwa nchini Ubelgiji.

kirusi kipya cha Covid-19 ambacho kimegunduliwa nchini Afrika Kusini, kinaweza kuambukia kwa haraka.
kirusi kipya cha Covid-19 ambacho kimegunduliwa nchini Afrika Kusini, kinaweza kuambukia kwa haraka. Guillem Sartorio AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kirusi cha B1.1.529, au Mu, kiligunduliwa nchini Afrika Kusini siku mbili zilizopita. Ni kirusi ambacho kinaambukia kwa haraka.

Profesa Tulio de Oliveira, mmoja wa watafiti, amepuuzia athari ya kirusi hiki kinachoweza kusababisha.

Wakati huo huo shirika la Afya Duniani, WHO, limeonesha mashaka dhidi ya kuweka vizuizi vya kusafiri kutokana na hofu ya virusi vipya vya Covid-19 aina ya B.1.1.529 likisema itachukua wiki kadhaa ili kuweza kubaini athari zake.

Shirika hilo limesema timu yake ya ushauri wa kiufundi kuhusu hali ya kugeuka kwa virusi (TAG-VE) ilifanya mkutano leo kujadili aina hiyo ya virusi ambayo imegundulika Afrika Kusini.Baadaye katika mkutano wake kwa waandishi wa habari msemaji wa WHO, Uswisi, Christian Lindmeier amesema shirika hilo linafuatilia kwa karibu mwenendo wa aina hiyo ya virusi, ambavyo taarifa za awali zinasema vina uwezo wa kubadilika mara nyingi na kusambaa kwa kasi zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.