Pata taarifa kuu

Omicron: safari za ndege za watalii kwenda Morocco zasitishwa

Kutokana na ainampya ya kirusi cha Corona cha Omicron, nchi mbalimbali zinatayarisha utetezi wao. Morocco imeamua kufuta safari za ndege kwenye ardhi yake kwa muda wa wiki mbili zijazo.

Hatua hii kali ilichukuliwa wakati Morocco, nchi ambayo utalii ni sekta muhimu ya kiuchumi, tayari imepiga marufuku raia wa nchi za kusini mwa Afrika kuingi kwenye ardhi yake baada ya kugunduliwa kwa aina mpya ya kirusi cha Omicron.
Hatua hii kali ilichukuliwa wakati Morocco, nchi ambayo utalii ni sekta muhimu ya kiuchumi, tayari imepiga marufuku raia wa nchi za kusini mwa Afrika kuingi kwenye ardhi yake baada ya kugunduliwa kwa aina mpya ya kirusi cha Omicron. FADEL SENNA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa kukabiliana na maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha Omicron, nchi mbalimbali zimechukua hatua. Siku ya Jumapili Novemba 28, mamlaka ya Morocco imetangaza kusitishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja za abiria kwenda na kutoka nchini humo. Sharti hili litaendelea kutumika kwa wiki mbili, kuanzia Jumatatu saa 5:59 usiku.

"Uamuzi huu unakuja kutokana na kuenea kwa kasi kwa aina mpya ya kirusi chaa Covid-19, Omicron, hasa Ulaya na Afrika, na ili kuhifadhi mafanikio yaliyopatikana na Morocco katika mapambano dhidi ya janga hili na kulinda afya za raia, " kamati ya ufuatiliaji wa mlipuko kutoka wizara mbalimbali imesema katika taarifa.

Tathmini ya hali hiyo "itafanywa mara kwa mara ili kurekebisha hatua zinazohitajika, ikiwa ni lazima," imeongeza taarifa hiyo. Masharti ya safari za ndege zinazoelekea nchi za kieni kwa abiria walio nchini Morocco kwa sasa hayajabainishwa. Hatua hii kali ilichukuliwa wakati Morocco, nchi ambayo utalii ni sekta muhimu ya kiuchumi, tayari imepiga marufuku raia wa nchi za kusini mwa Afrika kuingi kwenye ardhi yake baada ya kugunduliwa kwa aina mpya ya kirusi cha Omicron, iliyotambuliwa kwa mara ya kwanza kuambukia haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.