Pata taarifa kuu
MOROCCO-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Morocco yaweka karantini wakazi wa miji minane mikubwa ya nchi

Serikali ya Morocco imetanagza kufunga tena baadhi ya miji yake kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona na kuwataka wakazi wa miji hiyo kubaki ndani.

Maduka huko Marrakech yakiwa tupu kufuatia ya hatua ya serikali ya kuweka masharti ya watu kutotembea, Machi 16, 2020.
Maduka huko Marrakech yakiwa tupu kufuatia ya hatua ya serikali ya kuweka masharti ya watu kutotembea, Machi 16, 2020. AFP Photos/Fadel Senna
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya miji iliyotangazwa kufungwa kutokana na ongezeko hilo ni pamoja na Casablanca, Marrakesh, Fez na  Meknes.

Wakaazi katika miji hiyo wameagizwa kusalia katika miji yao, ili kusaidia kupambana na ongezeko la virusi hivyo ambavyo vimeonekana kuongezeka katika siku za hivi karibuni.

Hata hivyo, watu wanaosafirisha bidhaa muhimu kama chakula na dawa wameruhisiwa kuendelea na safari kutoka mji mmooja kwenda mwingine.

Serikali nchini humo imesema imerejelea hali hii kwa sababu wakaazi katika miji hiyo wameendelea kupuuza maagizo ya Wizara ya Afya kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi hayo.

Moroco kwa sasa ina visa zaidi ya Elfu 20 vya maambukizi, baada ya watu wengine karibu Elfu mbili kuambukizwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.